Uchaguzi 2020 Nimekerwa na kauli na Mgombea Ubunge mmoja kutamka hadharani kwamba hatopiga kampeni na atashinda

Uchaguzi 2020 Nimekerwa na kauli na Mgombea Ubunge mmoja kutamka hadharani kwamba hatopiga kampeni na atashinda

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nadhani kama kuna Jambo limekosewa ni kuwa na tume inayowapa uhakika Wagombea kwamba wafanye kampeni au wasifanye watapitishwa tu. Mmoja wa wagombea katika majimbo ya Mwanza amediriki kujinadi kwa marafiki zake kwamba Hana haja ya kampeni kwa sababu tayari ameakikishiwa ushindwa.

Anaeleza moja ya mkakati walionao ni pamoja na chama kutotumia gharama kubwa kuangaika na kampeni kwani utumie gharama au usitumie nafasi yako ipo pale pale. Anadai hii si kwa wabunge tu Bali Hadi madiwani na Urais.

Kwa kuongeza amediriki kusema Bora fedha wapewe wakururugenzi na wasimamazi wa uchaguzi Kama takrima kwa kazi nzuri wanayofanya kuliko kupoteza mafuta kujaza mafuta na kuwaonga wajumbe ambao baadhi yao hata kura awatapiga.

Hizi ni kauli zinatolewa adharani tena mbele ya Wananchi na anayetoa hizi kauli amesoma na kila siku anasikika akisema chama Cha wanyonge. Najiuliza hii mitano zaidi ndo mitano ya RUSHWA?
 
Leta ushahidi kama suo umbea wako tu?

Na kama ni kweli andika barua peleka tume ulalamike, usiposikilizwa subili asipofanya kampeni mpeleke mahakamani kutengua ushindi wake
 
Kwa wakati huu na Tume hii tuliyonayo, lolote linawezekana
 
Back
Top Bottom