Nimekoma kutumia Airtel Money.

sina hamu nao..kuanzia huduma yao ya blackbery inanitesa mpaka nalia........kujiregister tu masaa mia.........iyo eatel mane sijawahi jaribu maana toka nazaliwa na kukuzwa hatukufundishwa kupokea vya bure.
 

Ukishachukua pesa yako wapige chini. Wanaiga huku hawana wataalam.. Wanapeana tu ajira bila vigezo matokeo yao ndio haya ufanisi ni zero
 
Mi siandiki chochote kwa sasa maana usumbufu nilioupata na internet yao kama wiki 2 zilizopita haufai hata kusimulia, isitoshe hawana customer care kabisa, ni upuuzi mtupu. Nasikia ni wahindi ndo wanaendesha hii kampuni sahivi ndiyo maana ipo hivyo hovyo tofauti na zamani
 
kama upo jirani na huduma za benk afadhali utumie bank maana ni huduma ya kuaminika na ya uhakika kuliko longolongo za kwenye mitandao ya simu. hata ukidhulumiwa au ukipata usumbufu mkubwa hakuna hata kituo au mtu maalumu wa kushughulikia tatizo lako.

Wakati m-pesa inaanza kuna siku nilimtumia mtu hela kwa mpesa, ili mchukua kama wiki mbili kupata hiyo hela. hii mitandao imejaa wizi mtupu
 

Wamekataaa!!
 
Haya mambo ya kutuma pesa kwa njia ya mtandao haijatulia kabisa, bora turudi kutumia benki tulizozoea.
 
Hayo ni maoni na ushuhuda wa wateja wengi wa hiyo "eateli mane" au ukipenda Airtel Money! Binafsi nadhani ni ya kweli na yanaoyesha hali halisi ya aidha utapeli wa Airtel Money au uzembe na udhaifu katika kutoa huduma hii. Niseme jambo moja tu TCRA WAKO WAPI?Hebu waingilie hili na kulitatua mara moja.
 
Bahati mbaya hakuna mtoa huduma aliyekueleza kitu cha kweli! simple kumbuka hakuna huduma ya bure mjini
 
Airtel ni bomu sana, wamekuwa wanakata hela katika modem yangu wakidai mimejiunga na huduma za fiesta kitu ambacho si kweli. Hata baada ya kuongea na watu wa customer service hali hiyo imeendelea na nilipoenda Mlimani City nikakutana na mhusika ambaye hakunisaidia chochote.
 

utangoja sana ndugu yangu, mwenzio naenda mwezi wa 2 sasa, kila nkiwaambia naambiwa ombi lako linashughulikiwa nshajikatia na tamaa ya kuzipata tena hizo pesa.
 
utangoja sana ndugu yangu, mwenzio naenda mwezi wa 2 sasa, kila nkiwaambia naambiwa ombi lako linashughulikiwa nshajikatia na tamaa ya kuzipata tena hizo pesa.

Ha Princess Tee r u for real? Mimi tangu end of august nahangaika...kila siku napewa kumb. Namba...sijui lini tatizo litashughulikiwa. Apa nkipata tu ela yangu iliyomo uko nadhan statumia tena airtel money.

Ukipiga wanakuambia oh unajua sisi sio tunaotoa airtel money so tatizo lako ttalipeleka mbele..
Dah wamenchosha aisee.
 
Last edited by a moderator:
WalishindWa wakiwa na ZAP unadhani AIRTEL MONEY itaweza? VODA NA TIGO ndiyo mpaka vijijini.
hadi kesho huwa nasema airtel amechemka alikuwa atoke na zap lakini hakuipa promo na alikuwa peke yake sasa hivi anacheza makidamakida tu!........
 
Kuna lile tangazo lao la-imekatwa. Wa kawaida sana hawa jamaa.
 

Kaka shukuru kwamba hujapata. Mimi niliwahi kuibahatisha mara moja....nilijuta kuifahamu. Nikagundua kwamba mpokeaji HAKATWI lakini wewe mtumaji unakatwa mara dufu, kama wanakomoa. Na ukituma kuanzia laki 1 ndo mbaya zaidi maana wote mtumaji na mtumiwaji MNAKATWA. ndo maana ukiangalia matangazo yao wanataja vihela mbuzi kama Tshs. elfu 10, elfu tano, nk. hawathubutu kutangaza kwamba mtu katumiwa laki 2 halafu hajakatwa.

Lazima tujiulize, kama kweli ni bure....mtandao huu ungekuwa maarufu kuliko mingine, lakini hata wafanyabiashara hawautaki kwa kuwa hauna wateja. WANAKATA MNO.
 
Airtel wanapaswa ku-sweet talk the mawakala. Mawakala wakisusa mtandao kwa kutoweka flot, kwisha!
 
... Karibuni M-PESA.
Huduma iliyotulia kutoka mtandao uliotulia. Of course, the service can only be 99.9% perfect
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…