Nimekoma kutumia Airtel Money.


pole sana mkuu ndio uwezo wao huo tatizo ni kwamba bado haijakubalika kivile mujini..
 

Kwa kweli hilo tatizo limekithiri sana.Lakini mimi nadhani kampuni haina tatizo ila ni wale mawakala katika ufanyaji shughuli.Unajua wakati mwingine sisi watanzania ni wazembe sana katika biashara tunataka kujionyesha kwamba tunajua biashara wakati hakuna kitu.Mtu anaomba uwakala kwa umakini kabisa na kampuni inamuona huyu atafanya vyema hatimaye ankuwa mzembe.Sasa sijui ni mtaji unamuishia au nini.Kwa hili hatuko makini.Hata vocha za Vodacom ya shs 450 wanatuuzia 500.Ukimuukliza kwa nini unauza hiyo bei anasema hailipi tukiuza 450.Swali:Sasa si uache kuuza uuze vyenye faida na sisi kukandamiza wengine?
 
Usimshangae hy dada, ana royal customers wake hataki kuwapoteza kwa ww mpita njia, hujawai kuona ht maduka makubwa wanaacha kukuhudumia ww na kumhudumia aliyekuja baada ya ww, we ni mpitaji tu.
 
Watu mnadanganywa na vya bure. Hakuna kitu cha bure hapo. Kama ni bure wanapataje faida? Jiulize hilo swali kabla hujaliwa. So far, M-PESA ndio superior mobile money transfer service in Bongo. Nimeitumia mara nyingi sana na sina regrets kubwa sana ila inconvenience fulani pindi service inapokuwa down lakini ikirudi ni bien.
 
Ni bora kuachana na hiyo 'eatel mane,' inakatisha tamaa, kero nyingi. Nimemtumia mai waifu wangu elf 40, wakala kakata elf 2,kampa elf 38, kisa? anadai mtandao haumpi chochote? ndo aibe pesa za wateja? si aache kufanya nao kazi? pata picha kila atoaye chini ya laki 1 anakatwa elf 2, ni wizi ulioje?
 
Kumbe ndio ilivyo! Mimi nilifikiri nimesahau password ati, najuta sana kupadili password coz siwezi hata kumtumia mtu salio.

Ulifanikiwa kuifungua?
 

nilishalitupa li line lao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…