#COVID19 Nimekosa huduma ya afya kwakuwa sijapata chanjo. Je, chanjo ya COVID-19 ni lazima nchini Tanzania?

#COVID19 Nimekosa huduma ya afya kwakuwa sijapata chanjo. Je, chanjo ya COVID-19 ni lazima nchini Tanzania?

hazard Don

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Posts
1,203
Reaction score
1,007
Kwa mwenye kufahamu juu ya Hil naomba anifahamishe.

Nimekosa huduma moja ya kituo Cha Afya hapa nchini ,sababu sijachoma Chanjo ya COVID-19.

Je, hawa watoa huduma wamepata wapi jeuri ya kupinga kauli ya Mh. Rais

Ile kauli ya kuwa Chanjo sio Lazima.
 
Hawajitambui, hata kama wakisema lazima hawana chanjo za kutosha wala facilities kuwahudumia Watanzania wote.

Kuwachanja Watanzania wote 70% itachukua miaka, baadaye utahitaji pia booster. Wote watanyimwa huduma ya afya?
 
Mkuu tatizo ni pale umepata mgonjwa anayetakiwa kupatiwa huduma on time.
Unaambiwa mpaka upige Chanjo ya Covid.
 
ulikua unahitaji huduma gani mpaka ukaambiwa uchanje kwanza??

Tuanzie hapo kwanza.
Mrs. Ni mjamzito huwa Kuna taratibu za kuhudhuria kliniki.

So ile wameenda leo ,wameambiwa mpaka wachome Chanjo ya Covid, ndo wapatiwe huduma.
 
fanya mpango wewe na mkeo mkachanje ili kupunguza possibility ya kupata maambukizi ya Covid.
Hahaaa mkuu,umeongea kizalendo.
Nadhani kuchanja sio Tatizo, Tatizo ni kulazimishwa.
Kikubwa wao walete Chanjo za kutosha ili muda ukifika mtu akahitaji kuchanja ,Achanjwe kwa wakati.
 
Hahaaa mkuu,umeongea kizalendo.
Nadhani kuchanja sio Tatizo, Tatizo ni kulazimishwa.
Kikubwa wao walete Chanjo za kutosha ili muda ukifika mtu akahitaji kuchanja ,Achanjwe kwa wakati.
Unaonekana mnyonge sana, Mimi huo ujinga hawawezi kunifanyia.
 
Mwambie mke wako akachanje yupo kweny kundi ambalo ni kipaumbele hataki ajiudumie mwenyewe na ajifungulie uko uko ifike mahali mambo ya ku bembelezana yaishe ukikanyaga tu hospital unakutana na chanjo hutak ondoka full stop
 
Nitakapokosa plan B, nitafanya hivo.
 
Ndio yawezakua lazima,

Sasa tunaingia kwenye Zama za "NEW NORMAL" zikishapita hizi ulimwengu wetu utakua unadumbukia Sasa kwenye "NEW WORLD ORDER"

Ni Nini New Normal?

Hiki Ni kipindi ambacho suala la Corona litakua Ni kitu Cha kawaida "Normal"

Na kwa mujibu wa taratibu Kila taasisi itakua imeweka ulazima wa Kila mpata huduma kuchanja then kwa ugumu huo Kila mtu atalazimika kuchanja kwa muda wake na Kila mtu ataona Ni kitu Cha kawaida "normal" na maisha yataendelea

Ukirejea baadhi ya hotuba za George Bush, hasa hutuba yake maarufu ya AMERICA IS UNDER ATTACK, Baada ya shambulio la September 11

Bush alibainisha kwamba NEW WORD ORDER Ni suala la lazima

Na akamalizia kuionya dunia kwamba kwenye harakati zao "you will choose to be in our side... Or the side of the terrors!

Akimaanisha kwamba dunia lazima ichague ama kua upande wa wamarekani ama kua upande wa magaidi

Kwa hiyo kiongozi tulia uchanjwe, tupo kwenye Zama za new normal kuelekea N.W.O
 
Back
Top Bottom