DOKEZO Nimekosa huduma ya Meli ya MV. Victoria, inadaiwa haifanyi kazi wiki ya pili sasa, Mamlaka mbona mpo kimya?

DOKEZO Nimekosa huduma ya Meli ya MV. Victoria, inadaiwa haifanyi kazi wiki ya pili sasa, Mamlaka mbona mpo kimya?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kuna taarifa ya kuwa Meli ya MV. Victoria imesitisha kufanya safari kwa takribani wiki mbili sasa, hiyo ni baada ya kupata hitilafu kwenye mfumo wa uendeshaji lakini mamlaka inayohusika ya Tanzania Shipping Company Ltd (TASHICO) imekuwa kimya.

Ni kweli kuhusu taarifa hizi? Maana inadaiwa kuna watu wanahaha kupata usafiri wa Mwanza - Bukoba.

Ufafanuzi zaidi soma hapa
~
TASHICO: Ni kweli huduma za Meli ya MV Victoria zimesimama kwa ajili ya service ya kawaida
~ TASHICO: MV. Victoria itaendelea kusimamisha huduma kwa muda wa mwezi mmoja kwajili ya kufanya 'service'
206164054_1225568667874932_6296371288849066999_n.jpg

thumb_753_800x420_0_0_auto.jpg


Pia soma
~
Meli ya MV. Victoria (Mwanza) haina crane ya kubebea mizigo zaidi ya miezi miwili, ni hujuma?
~ MSCL: Ni kweli mtambo wa kubebea mizigo wa MV Victoria ulipata hitilafu ya kiufundi
 
Kuna taarifa ya kuwa Meli ya MV. Victoria imesitisha kufanya safari kwa takribani wiki mbili sasa, hiyo ni baada ya kupata hitilafu kwenye mfumo wa uendeshaji lakini mamlaka inayohusika ya Tanzania Shipping Company Ltd (TASHIBA) imekuwa kimya.
TASHIBA wameshashiba hawajali tena!
 
Hii meli safi sana! Pale bar siku hiyo nikakutana na wafanyabiashara wa Uganda tukaanza kula Konyagi huku bendi ikiimba nyimbo za kale mpaka mid nights
 
Back
Top Bottom