Nimekosa kibarua kisa kitambulisho cha Taifa. Ni Mwaka wa nne sijapata kitambulisho cha NIDA

Elias K

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2021
Posts
213
Reaction score
607
Wakuu Kama mmesoma threads zangu za nyuma, ni wazi kwamba napitia kipindi kigumu kimaisha. Sasa wiki hii Kuna kibarua nilipata hapa Arusha wakahitaji kadi ya nida na ya chanjo ya Corona, nikawapa ya Corona na namba ya NIDA, wakasema wanahitaji kadi kabisaa siyo namba!

Nilijiandikisha tangu mwaka 2019 katika kituocha USA-river, Arusha. Ajabu ni kwamba Kuna baadhi ya watu nawafahamu walijiandikisha mwaka jana(2021) na tayari Wamepata vitambulisho. Najiuliza wamavipataje mapema hivyo!

Leo nimeenda pale ofisini saa mbili na nusu, ofisi ipo wazi ila wahusika hawajafika kazini. Baadaye walipofika, majibu ni yale yale "kitambulisho chako bado hakijatoka, kikitoka utajulishwa.

Nikawaambia naomba Kama Kuna utaratibu sikukamilisha mniambie tu nijaze fomu upya kwani kuna wenzangu wameshapata na nilijiandikisha kabla yao, wakasema "fomu lako limekamilika kabisa endelea kusubiri tutakupigia simu"

Najiuliza tu kama hao ni watumishi wa umma au ni akina Nani. Na ilikuwaje waliojiandikisha mwaka 2021 wameshapata kadi zao lakini Mimi niliyejiandikisha mwaka 2019 sijapata Hadi wa leo?! Au ndiyo Mambo ya connection?! Nimewaza hivyo baada ya kusoma baadhi ya nyuzi ambazo nitaziambatanisha hapa chini.

Kama Kuna mtu anaweza kunisaidia aninisaidie tafadhali, hata ukihitaji chai nitakupa ilimradi nipate hiyo kadi nikakamilishe maombi ya kazi.

Pole sana mkuu ndio matatizo ya kuishi in a shithole country, hii ilitakiwa isitokee kama serikali ya Nyerere ingeendeleza na kuboresha uwezo wa serikali wa kutambua raia wake, kikawaida ilitakiwa kwa umri huo uwe na ID long time ago, inavyotakiwa mtoto anapozaliwa tu, within few minutes wazazi wanakua wameshampa Jina mtoto wao ili atambulike na serikali ilitakiwa within 14 pia impe mtoto huyu jina(ID number )ili mtoto akifikisha 18yrs apewe ID yake au life book;nothing unaweza kufanya,maana uoga umetamalaki huwezi kufanya ile one man stand, yaani ingia ofisi ya NIDA na goma kutoka hadi upate ID book au mteke ofisa yeyote hapo wa Nida, huwezi endelea kusubiri na kulalamika humu.
 
Ahsante
 
Ningeomba msaada kwa wale waliopata changamoto kama ya kwangu waliitatua vipi...ilikuwa 2017 nikawa oparator wa yale mashine za kujisajilia Nida....changamoto ikaja kwamba kuna wale watu fingerprint hazisomi...sasa wale oparators wakuu wakawa wanatuambia tuwasaidie kuweka hata kidole kimoja au viwili ili kukamilisha taarifa....Sasa changamoto inakuja kuwa namba haijarudi na nmejaribu kufuatilia wananambia kuwa taarifa zangu zimeingiliana na mtu mwngine na natakiwa nimlete huyo mhusika ili waweze kubadili taarifa kitu ambacho ni vigumu kumpata mhusika huyo..natanguliza shukran kwa yule atakaeweza kunisaidia kweny hili kwan nishafuatlilia sanaa bila mafanikio
 
Wakuu Kama mmesoma threads zangu za nyuma, ni wazi kwamba napitia kipindi kigumu kimaisha. Sasa wiki hii Kuna kibarua nilipata hapa Arusha wakahitaji kadi ya nida na ya chanjo ya Corona, nikawapa ya Corona na namba ya NIDA, wakasema wanahitaji kadi kabisaa siyo namba!

Nilijiandikisha tangu mwaka 2019 katika kituocha USA-river, Arusha. Ajabu ni kwamba Kuna baadhi ya watu nawafahamu walijiandikisha mwaka jana(2021) na tayari Wamepata vitambulisho. Najiuliza wamavipataje mapema hivyo!

Leo nimeenda pale ofisini saa mbili na nusu, ofisi ipo wazi ila wahusika hawajafika kazini. Baadaye walipofika, majibu ni yale yale "kitambulisho chako bado hakijatoka, kikitoka utajulishwa.

Nikawaambia naomba Kama Kuna utaratibu sikukamilisha mniambie tu nijaze fomu upya kwani kuna wenzangu wameshapata na nilijiandikisha kabla yao, wakasema "fomu lako limekamilika kabisa endelea kusubiri tutakupigia simu"

Najiuliza tu kama hao ni watumishi wa umma au ni akina Nani. Na ilikuwaje waliojiandikisha mwaka 2021 wameshapata kadi zao lakini Mimi niliyejiandikisha mwaka 2019 sijapata Hadi wa leo?! Au ndiyo Mambo ya connection?! Nimewaza hivyo baada ya kusoma baadhi ya nyuzi ambazo nitaziambatanisha hapa chini.

Kama Kuna mtu anaweza kunisaidia aninisaidie tafadhali, hata ukihitaji chai nitakupa ilimradi nipate hiyo kadi nikakamilishe maombi ya kazi.

NIDA badala ya kuja kutatua tatizo la Vitambulisho kwa Wananchi wa Tanzania imekuja kuongeza tatizo lingine mpya ambalo halikuwepo hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa NIDA.
NIDA ni Kero kubwa sana kwa waTanzania.
NIDA imekuwa Janga la kitaifa
 
Labda sio raia mkuu na unatiliwa mashaka. Joking tu 😅😅

Hebu nenda ofisi za kanda kule kisongo. Mbona wengine ndani ya muda mfupi tu wanakuwa wameshapata namba?

Sema watanzania sisi hatupo serious kwenye mambo mengi sana hili la nida ni moja wapo.

Raia kisa ana namba hafuati kitambulisho, nida nao sijui mitambo yao imekufa. Maana idadi imepungua raia kama huyu anateseka kupata kitambulisho.
 
Back
Top Bottom