Columbus
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 2,002
- 651
Baada ya kufanyiwa kazi fulani na kukamilika nilipatiwa namba na wafanyakazi hao ili nimtumie bosi wao malipo kwa njia ya M-pesa, kwa bahati mbali walinipatia namba ya mtu mwingine kwa makosa na hivyo fedha kumuendea mtu huyo. Baada ya kuwasiliana na Vodacom huduma kwa wateja walinijulisha kuwa huyo niliyemtumia hizo fedha ameshazitoa toka kwa wakala.
Baada ya mtu niliyemtumia fedha kutokuwa hewani kwa muda mrefu hatimaye aliwasha simu na nikaweza kuongea naye, alikubali kupokea fedha hizo na kuzichukua lakini aliniahidi kunirudishia. Pamoja na kumtaka achukue kiasi cha sh. elfu kumi(Tsh 10,000/- kutoka ktk fedha hizo kwa usumbufu alioupata, hata hivyo amekuwa akinibabaisha na kuzima simu yake muda mwingi na hivyo nimeona ananikwepa, Hivi kuna namna nyingine yoyote ya kuzipata fedha hizi au ndio basi tena! naomba mawazo yenu.