Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Gentamycine juzi aliandika humu baada ya Pablo kufukuzwa Simba kuwa baada ya Matola kupewa timu, basi gemu zote 5 atashinda, kweli bwana, soka wanalocheza Simba kiukweli huwezi amini kama ndio wao walioshika nafasi ya 2, mpira unapigwa mwingi sana, yaani mpira unapigwa unafurahi, wale wachezaji wa benchi akina Nyoni wanaupiga mwingi hadi unamwagika, kweli ni uwezo wa Matola au mipango nje ya uwanja anaijua, nakubaliana na Gentamycine kuwa Matola 'mchawi'.