Nimekukubali Gentamycine, Matola 'mchawi'

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Gentamycine juzi aliandika humu baada ya Pablo kufukuzwa Simba kuwa baada ya Matola kupewa timu, basi gemu zote 5 atashinda, kweli bwana, soka wanalocheza Simba kiukweli huwezi amini kama ndio wao walioshika nafasi ya 2, mpira unapigwa mwingi sana, yaani mpira unapigwa unafurahi, wale wachezaji wa benchi akina Nyoni wanaupiga mwingi hadi unamwagika, kweli ni uwezo wa Matola au mipango nje ya uwanja anaijua, nakubaliana na Gentamycine kuwa Matola 'mchawi'.
 
Nilishasema mara nyingi humu. Kama Simba wanashindwa kumuondoa Matola angalau wampatie kitengo kingine.

Kwasasa jamaa anainfluence kubwa kwa wachezaji. Sishangai kocha atakayefuata akifeli. Bongo ndio sehemu pekee ambayo kocha mkuu unachaguliwa kocha msaidizi.
 
Hata huko walikoendelea kisoka huwa inatokea kocha mkuu kuchaguliwa kocha msaidizi.

Nakupa mfano Ajax amsterdam.
 
Sasa timu imebakiwa na mechi 3 tu kumaliza ligi! Kuna dalili ya wachezaji wengi kuachwa!

Unategemea hao wanaopata nafasi wacheze chini ya kiwango? All in all, haisaidii chochote! Bingwa alishapatikana kitambo.
Binafsi nafurahi sana hao wazee wanavyofanya vizuri ili waaminiwe wapewe mikataba mipya ili tuendelee kujipigia hao makolo
 
Humu JF hakuna Prof. wa JF, hakuna Dr. wa JF ila mimi nimemtunuku PhD ya JF, ndio maana namwita Dr. GENTAMYCINE.
 
Mafanikio yao hao waliofukuzwa yanasomekaje?
 
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Tunu ( Shani ) zake nyingi alizonitunuku na kunifanya niwe Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer hapa duniani.

Cc: adriz
 
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Tunu ( Shani ) zake nyingi alizonitunuku na kunifanya niwe Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer hapa duniani.

Cc: adriz
Siku hizi umebadilika mkuu umepunguza undava, kuna mwaka kulikuwa na mechi ya Taifa stars ukatabiri ili ishinde kwenye first eleven asikosekane Fei na Ajibu na wakiwepo mechi itaisha mbili bila na goli la kwanza atashinda Fei, watu walikushambulia sana baadae mocha alipanga kama ulivyosema na na Fei alianza kushinda na mechi ikamalizika mbili bila.

Baadae ulirudi kwenye uzi na moto wa mashambulizi na tambo kisha kuanza kuwapopoa wote waliokudhihaki na waliokuja kutoa pongezi za kinafki.
 
Naona umejifungulia uzi ili kujisifia
 
Kwanza niwapongeze mleta mada kwa kutukumbusha aliyotabiri Genta na Genta mwenyewe kwa kuona mbali.

Hili jambo nadhani viongozi wasilichukulie kirahisi inabidi walifanyie "homework" ili ijulikane hasa nini kilikuwa nyuma ya pazia. Haiwezekani timu ilikuwa "slow" sana ikawa "ina struggle" kupata ushindi hata kwa timu ndogo leo hii inashinda kirahisi sana huku ikicheza kwa kasi na pasi za uhakika. Je ilikuwa hujuma? au wachezaji walikuwa hawamtaki kocha? au mbinu za kocha zilikuwa mbovu?

Bila uongozi kufanya kazi ya ziada na kutafuta nini kilikuwa sababu ya msingi timu kufanya vibaya na ni nini hivi sasa kinasabaisha timu imeanza kufanya vizuri basi wajue tu msimu ujao yanaweza kujirudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…