Nimekukumbuka dada yangu Dena Amsi

Nimekukumbuka dada yangu Dena Amsi

Mgugu

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
2,165
Reaction score
4,403
Tokea jana kila nikiingia Jamii forum najikuta moyo wangu unakua mzito, nafasi yangu inakosa raha, simanzi na huzuni inatawala ndani ya moyoni wangu,
Nakumbuka jinsi ulivyokua mkarimu kwangu na kwa wanajamii forum wote hususan katika hili jukwaa letu la MMU.
Upole wako, ucheshi wako, michango yako yenye busara na zaidi ni ushauri wako juu yangu kila nilipokua napitia katika changamoto mbalimbali.
Kila nikiiona avatar na michango yako humu jukwaani maumivu ya kidonda moyoni mwangu huanza upya.
Pumzika kwa amani dada yangu, sote njia yetu ni moja tumeumbwa kwa udongo na tutarudi kwa udongo.
Innaalillahi wainnaa ilaihi raajiuun.

Sent from my GT-P5200 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom