Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Kama miaka ingekuwa inarudi nyuma, basi ningeirudisha ili nione wababe hawa wawili ambao wametangulia mbele ya haki walivyokuwa wakiumizana pale katikati ya dimba, ubabe sio wa kawaida.
Simba ilipokuwa ikicheza na Nyota Nyekundu, watoto wa kariakoo wote hao kazi ilikuwa ngumu sana, Roster alikuwa mkorofi sana, mhuni na mbabe.Hakuwa na tofauti na marehemu Idd Seleman Kibode au Nyigu.
Dimba la kati lilichafuka haswa huku refa akiwa busy kuwaangalia jamaa hao wawili wakitoleana maneno machafu, vitisho na kadhalika.Wengi wanaona battle ya Gaga na Athuman China ndio ilikuwa kali lakini sio kweli, Roster Ndunguru na Hamis Gaga Gagarino ilikuwa battle tamu sana.Mpira ukiisha bado wanatishia maisha.