Nimekumbuka 'battle' ya marehemu Hamis Gaga na Roster Ndunguru

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kama miaka ingekuwa inarudi nyuma, basi ningeirudisha ili nione wababe hawa wawili ambao wametangulia mbele ya haki walivyokuwa wakiumizana pale katikati ya dimba, ubabe sio wa kawaida.

Simba ilipokuwa ikicheza na Nyota Nyekundu, watoto wa kariakoo wote hao kazi ilikuwa ngumu sana, Roster alikuwa mkorofi sana, mhuni na mbabe.Hakuwa na tofauti na marehemu Idd Seleman Kibode au Nyigu.

Dimba la kati lilichafuka haswa huku refa akiwa busy kuwaangalia jamaa hao wawili wakitoleana maneno machafu, vitisho na kadhalika.Wengi wanaona battle ya Gaga na Athuman China ndio ilikuwa kali lakini sio kweli, Roster Ndunguru na Hamis Gaga Gagarino ilikuwa battle tamu sana.Mpira ukiisha bado wanatishia maisha.
 
Kama miaka ingekuwa inarudi nyuma, basi ningeirudisha ili nione wababe hawa wawili ambao wametangulia mbele ya haki walivyokuwa wakiumizana pale katikati ya dimba, ubabe sio wa kawaida...
Usitutishe🤪
 
Kiungo red star walikua muhidini pazi na Stephen chibichi. Vitasa kuna Abas kuka na Frenk Kasanga.
Juu kuna John Mgazija na Mohamed Mgarike (jitu kubwa)
Roster Ndunguru winga namba 7.

Gaga alikua namba 8 pale msimbazi labda wakutane marachache sana kwenye baadhi ya maeneo uwanjani, kwakua position zao haziwafanyi wakutane marakwamara.
Rosta Ndunguru alikua muanzishaji mkubwa wa fujo uwanjani japo alikua mfupi.
Niliwahi shuhudia akianzisha ugomvi kwa kumtandika refa pale shamba la bibi.
 
Mi ni kijana Mdogo.

Kati ya.

Sunday Manara.

Kitwana MANARA.

Hamis Gaga. Na

Abdallah kibadeni.

NI NANI MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA????

GOAT.
 
Dah umenikumbusha mbali sana aisee, huyo Jamaa Roster Ndunguru alikuwa machachari na mbabe balaa hata nywele alikuwa hachani (Kipindi hicho kutochana nywele ilikuwa ni utovu wa nidhamu).
 
Mi ni kijana Mdogo.

Kati ya.

Sunday Manara.

Kitwana MANARA.

Hamis Gaga. Na

Abdallah kibadeni.

NI NANI MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA????

GOAT.
Gaga mtoe apo, Gaga alikua mchezaji mzuri kiasi yupo kwenye kundi la akina Marsha, china, Ngurungu n.k wachezaji wazuri kiasi katika kizazi chao ila ingekua kwenye kizazi cha sasa wangekua nyota wakubwa.

Tukirudi kwenye mada Sunday baba yake Haji alikua habari nyingine na kwamiaka iyo alipewa Nickname ya computer.
 
Mi ni kijana Mdogo.

Kati ya.

Sunday Manara.

Kitwana MANARA.

Hamis Gaga. Na

Abdallah kibadeni.

NI NANI MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA????

GOAT.
niliwai kumuuliza swali kama hili legend Makumbi Juma"homa ya jiji",mchezaji gani wa zamamani alikua mzuri kuzidi wengine?" akanitajia Hamis Gaga alikua mahili sana.

Shida iliyopo hakuna video za kumbukumbu za kuwaona hao tunaoambiwa mfanano yao uwanjani ni kama kina Zidane na Ronadinho.
 
Huwa nawaambia ukisimuliwa jitahidi utafute ukweli. Hamis Gaga "Gagarino" alikuwa kiungo wa mbele "Attacking midfield" wakati Roster Ngunguru akicheza winger ya kulia kipindi hicho wachambuzi wakiita "outside right". Kwa ufundishaji uliokuwepo mchezaji kama Roster hata Ku cut in ilikuwa nadra Sana. Hivyo ukinambia alikuwa anapambana na Gaga utakuwa umetupanga Mkuu.
Wapinzani wakubwa wa Roster alikuwa Twaha Hamidu "Noriega" Kwa upande wa Simba na Fred Felix Katarahiya Minziro aka Baba Isaya.
 
Mi ni kijana Mdogo.

Kati ya.

Sunday Manara.

Kitwana MANARA.

Hamis Gaga. Na

Abdallah kibadeni.

NI NANI MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA TANZANIA????

GOAT.
Kwangu Sunday kama mchezaji ni GOAT, Kibadeni ana mafanikio ya kuwa mchezaji mzuri na kocha mwenye mafanikio.
Sunday ni miongoni mwa Wachezaji wa awali Tanzania kucheza mpira wa kulipwa Ulaya. Pia ni Kati ya Wachezaji wachache waliobadili position ya uwanjani na bado akapata mafanikio. Alitoka kipa kuwa forward.
 
Humjui Roster Ndunguru wewe, yaan mm nisimuliwe, haya Mohamed Mgalike sijamuona, Faustine Chibingwa sijamuona, John Bosco sijamuona, Habib Kondo sijamuona, Abunu Issa sijamuona? We choko kweli
 
Nadhani yeye alikutajia Kati ya aliocheza nao.
 
Umeongea facts, ila nimeshuhudia sana Gaga akigombana na Roster.Umemsahau Abunu Issa, enzi hizo tulikuwa na akina Malboro na Mkama Shapu, pingu, virungu, pisto kila silaha alikuwa anayo mwili, mbwa walikuwa ulinzi mkubwa uwanjani hasa upande wa uwanja wa mkapa ss hv, eneo lilikuwa wazi.
 
Upo upo sahihi
 

Attachments

  • 048B997F-84A3-4251-A0C3-B69AD3BF8A74.png
    67.8 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…