Nimekumbuka hii nikacheka sana; tuliowahi kukojoza kitandani tukiwa boarding njooni tutoe ushuhuda

Ila inasemekana kikojozi hasinzii ugenini. Ya kweli hayo?!
 
Aisee hakuna kitu kimenusumbua kama hicho nillikuwa napigwa bakora na bro acha kabisa.
Ila nakumbuka darasa la tano Mother alimuambia bro aache kunichapa kwa sababu sio kosa langu hakuna anayependa kukojoa ila inatokea bahati mbaya.

Mother kuna ushauri alinipa ambao pia niliwasaidia wengi wakaacha kukojoa
Ngoja niwape hapa ili msiwachape watoto wenu ila muwashauri kama alivyonishauri mimi Mother wangu na kunisaidia kabisa kuacha kukojoa nikiwa darasa la tano.

Aliniambia ya kwamba nihakikishe kuanzia asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ninywe maji mengi ya kutosha.
Itapofika kuanzia saa moja usiku nisiguse maji wala kimiminika chochote
Nifanye hivyo ndani ya mwezi then niendelee na utaratibu wangu wa zamani.
Nilifanya hivyo ndani ya mwezi kama alivyonishauri bi mkubwa toka siku hiyo naanza huo utaratibu sikuwahi kukojoa tena kitandani kitu ambacho nilijifunza kukojoa ni saikoloji hata zile ndototo pia ni saikoloji pia.

Ndio maana mimi nilifuata ule utaratibu wa mother ndani ya mwezi means ili kuujengea ubungo mazoea na hata baada ya mwezi kuisha nilivyoanza kunywa maji usiku pia sikuwahi kukojoa tena coz tayali nilishaweka mazoea kwenye akili yangu.
 
Nimawatoto wanakojoa mno, ngoja nijaribu kuwalea kwa hii mbinu nione..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…