Bulelaa
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 1,342
- 3,247
Enzi za (JPM) hata aliyekuwa kilaza wa siasa, alivuma
Enzi za JPM, kila raia alikuwa akitamani kushinda kwenye luninga akiangalia matukio ya siku hiyo
Huku mzee wa kuwasukuma ndani aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora mzee Mwaniri, alichangamsha mkoa huo
Dar es salaam akiwapo kijana maarufu kuliko hata mawaziri (baadhi) na siyo wote bwana Paul Makonda, alilichangamsha jiji
Kule Hai akiwako kijana machachari aliyeishia jera bwana Lengai, acha buana, Mzee Lema alotamani ahame mkoa
Kijana wa Kizaramo kipindi hiko akiwa Waziri wizara ya TAMISEMI mh. Jafo, mbona siasa ilikuwa moto? kwa namna ya alivyokuwa akienda, binafisi nalianza kumpa nafasi ya yeye siku moja aje kuwa Rais wa nchi hii, huyu kijana ni alikuwa moto, nilimkubali na kumkubali haswaa
Waziri wa Sheria na mwalimu wa mambo sheria na katiba mzee wetu mh.Paramagamba Kabuudi, jina murua kabisa hili, binafsi nampenda tu huyu mzee, ni muwazi, msomi na mwenye kujiamini sana, heshima kwako mzee wetu na uishi milele, alikuwa waziri na kutumika kama mwalimu hapo mjengoni!
Waziri mkuu enzi hizo na sasa akiwakilisha vema kabisa, mh Kassimu Majaliwa Kassimu! Ulindwe na Mungu mkuu,
Akiwepo sasa na aliyekuwa kiranja wao na Rais wa Jamhuri ya watu wa Tanzanian mh. Dr. Joseph Pombe Magufuli (RIP) hakika, tulianza kuiona TANZANIA ikielekea kuzuri zaidi,
Uhamasishaji uliokuwepo kuhusu kujitoa kwa kila Mtanzania kwa kufanya kazi kwa juhudi kubwa huku wakiongozwa na uzalendo, tuliona mabadiriko makubwa yakitokea kwa kasi kwenye maofis ya umma karibu yote
Watumishi wa Umma wakiendana na kasi ya awamu hiyo,
Mbali na hayo yoyote, mazuri huwa hayakosi changamoto, yapo mengine yaliwaumiza baadhi ya Watanzania wenzetu wakajikuta wakichukuzwa zaidi na uongozi huo mpaka hivi leo
Lakini kwa uwingi wa watanzania walipenda sana na kuchangamshwa na staili ya siasa ilivyokuwa ikifanywa
Hii staili ya siasa enzi hizo, natamani tena ijitokeze huko mbeleni
Naamini, Tundu lissu akishika madaraka, siasa za kipindi cha JPM zitarudi kwa kasi ikiwezekana kuzidi kiwango chake JPM
Mungu Ibariki TANZANIA
MUNGU wabariki viongozi wote wenye nia njema na nchi yetu Tanzania