Nimekumbuka wimbo wa Chidi Benz uitwao 'Mmenisoma?'

Atapona tu...wabongo wanapenda sana MTU akiwa na matatizo
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Atakua pia hajasikia Uswahilini Matola-Kosa la Marehemu.
 
kabisa,huo wimbo ulikuwa wimbo wa taifa enzi hizo tv pekee ni ITV
Hahahaha shooting nyuma kuna kitambaa cha bluu kimetandazwa na ndiyo background hiyo hiyo.

Jela ya Fm Academia (Wajela jela) na yenyewe shooting yao ilikua hivi.
 
Hahahaha shooting nyuma kuna kitambaa cha bluu kimetandazwa na ndiyo background hiyo hiyo.

Jela ya Fm Academia (Wajela jela) na yenyewe shooting yao ilikua hivi.
Shooting ilikuwa inafanyika hapohapo studio na nyimbo zinakuwa za Taifa, sahivi video hadi ibambe sharti utumie Red Camera kwa Hanscana ama uende kwa Madiba, maisha yanaenda kasi
 
Shooting ilikuwa inafanyika hapohapo studio na nyimbo zinakuwa za Taifa, sahivi video hadi ibambe sharti utumie Red Camera kwa Hanscana ama uende kwa Madiba, maisha yanaenda kasi
Sana aisee, 2 eyez production na royal production ndiyo walikua wanashindana.

Mwananchi video production alibase kwenye muvi ila ile video ya Nakupenda ya Abby Skills, Zahrani na Dully ikawa imeleta kitu chenye msisimko sana
 
Hapa tunasubiria ulimwengu uanze shule yake maana hakunaga namna nyingine hapo
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Ongezea na hizi;
Fad-moyoni naumia
Shetta-Mdananda
Solid Ground Family-Mechi Kali
Jebby-marehem kaacha orodha
Joslin-mshkaji mmoja
 
Hii nyimbo aliitoa baada ya kuchukua tuzo mbili za hip hop kwenye KTMA na watu kumdisi sana kuwa hakustahili kwa kuwa hakuwa hajulikani sana. Jibu lake ndo hilo 'MMENISOMA'
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Mkuu nilisema kwangu mimi...that's means kila mtu Ana mtazamo wake.

Narudia tena kwangu mimi huu ni wimbo bora kuhusu janga la ukimwi pembeni ya starehe na Alikufa kwa ngoma hizo ulizotaja wewe zitashika nafasi ya 4 na kuendelea ila tatu bora yangu ni Alikufa kwa ngoma,Starehe na Mmenisoma.

Kama natengeneza top 5 nitaiongeza Zawadi ya Late Mangwea na ngoma ya Solid Ground Family inaitwa Mechi Kali.
Hivyo yaani.
 
Ile freestyle ya matusi mazito mazito hujaikumbuka? Uhai, mafanikio na afya huwa vinatupumbaza sana waja tunasahau kavitoa nani!
 
Ujafa ujaumbika inasikitisha MTU aliesimama vizuri kwenye sanaa Leo anakuwa teja, tumuombee arudi hali ya kawaida,yeye nae hakuwahi tukana watu kwenye kampeni Leo ye mgonjwa walotukanwa wazima,tusiringie afya ni ya Mwenyezi Mungu
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Brother huu wimbo wa Mpiga Debe unao unisambazie upendo Mkuu?

"Kupiga debee kwangu ilikuwa poa, fani katika maisha ikaja kuniokoaaaa... Kwa hadhi ya wazazi kijijini nika oa......."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…