Huu wimbo ulinifanya nimuheshimu sana Chid.
Beat nzuri kutoka kwa Goodfather P.Funky Majani ilibebwa na sauti nzito yenye mamlaka kutoka kwa Chid Benzino.
Verse anazungumzia starehe tu na kujiachia viwanja na hata wenye dawa mfukoni anawapa ruksa wanyonge fresh tu.
Ila verse ya pili na ya tatu anabadilika kabisa kama sio yeye anazungumzia UKIMWI kwa namna ya kipekee kabisa ambayo itakuacha na mstuko.
Mtu aliekwambia muende club,kuruka majoka na kuvuta bange anakuhusia kuhusu ukimwi.
ukiondoka Alikufa kwa Ngoma ya FA na Starehe ya Feroos Huu ndio wimbo bora zaidi wa UKIMWI kwenye bongo flava.
Kwangu Huu ndio wimbo bora zaidi kutoka kwa Rashidi pembeni ya Dar es Salaam stand up na Hasira za nini