Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
TUHUMA za matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 100 ndani ya klabu ya Yanga zimechukua sura mpya baada ya katibu mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako kueleza kuwa alikuta fedha kidogo kwenye akaunti ikilinganishwa na zile zinazodaiwa kufujwa.
Mwalusako ambaye hakutaka kukiri kufujwa kwa fedha hizo au la, alieleza kushangazwa na ufujaji huo wa fedha na kutaka suala hilo aulizwe aliyekuwa katibu mkuu , Lucas Kisasa kwa kuwa ndiye anayehusika moja kwa moja.
"Tangu niingie madarakani kila kitu kinakwenda sawa, ila hizo fedha mimi sikuzikuta ,sijui chochote kuhusu hilo kama zilikuwepo au la.
Kisasa ndiye aliyekuwa mtendaji ni vema akaulizwa yeye, ninatumaini atakuwa na majibu ya kutosha kuhusu fedha hizo.
"Kimsingi, mimi siwezi kujua undani suala hilo kwa sababu klabu pia ina matumizi yake ya hapa na pale, hivyo ukimtafuata (Kisasa), bila shaka utapata ufafanuzi wa kutosha,"alisema Mwalusako.
Hata hivyo, Kisasa alipotafutwa kwa simu zake mbili za mkononi, hazikuwa na majibu zaidi ya kuita bila kupokewa.
Mwalusako, kwa upande wake aliongeza kuwa ni kweli wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wamekuwa wakitoa michango yao kila kukicha, lakini hadhani kwamba michango kama inaweza kufikia kiasi kilichotajwa.
Alisema kuwa yeye ni katibu wa kuajiriwa ambaye anafanya kazi kwa misingi ya katiba ya klabu ya Yanga na kwa kuifuata maelekezo ya kamati ya utendaji, hivyo hana shaka kwamba kila kitu kinaenda sawa tangu alipotwaa madaraka.
"Mimi ni katibu wa kuajiriwa wa klabu ya Yanga nafanya kazi kwa kufuata katiba iliyopo na pia kupokea maelekezo kutoka kamati ya utendaji, sasa katika hilo sina shaka hata kidogo kwamba kila kitu kinakwenda sawa tangu nilipoingia madarakani,"alisema.
Jana, Mwananchi iliripoti kwa mara ya kwanza tuhuma za baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuutaka uongozi wa klabu yao chini ya mwenyekiti, Imani Madega kuweza wazi kuhusu fedha za malipo ya kadi za unachama zinazodaiwa kufikia mlioni 100.
Hata hivyo, Madega aliiambia Mwananchi kuwa ni majungu ambayo yamekuwa yakienezwa kwa lengo la kuonyesha kuwa uongozi wake umetumia vibaya fedha za ada ya uanachama wa klabu hiyo.