Nimekuta namba yangu ya Tigo niliyotumia miezi mitatu iliyopita imebadilishwa usajili, whatsapp yangu imebadilishwa ?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Leo nikiwa natumia whatsapp nimekuta picha ya namba yangu ya Tigo kuna mtu mwengine kajipiga selfie

Naenda kuangalia usajili wa majina kwa njia ya kutuma pesa nakuta majina tofauti.

Hili jambo limenishangaza sana juu ya privacy ya namba zangu, kwa bahati nzuri haikuwa namba nayotumia sana.

Kwanini hatupewi taarifa pale namba zetu zinapobadilishwa usajili ?
 
Jambo hili linapaswa kutazamwa tena upya kutokana na unyeti wake.

Ni lazima kabisa Serikali kupitia TCRA iweke Wazi kabisa kuhusu HAKI na WAJIBU wa Wamiliki hao tofaufi wa SIM Card kuhusiana na masuala haya ya kubadilisha Mmiliki wa SIM Card za simu kwa sababu suala hili linahusisha Usalama wa Taifa. Tukumbuke kwamba, suala la Usalama wa Taifa zima linaanzia na Usalama wa mtu mmoja mmoja katika Jamii.
 
Ila kwa kweli haya mambo ya laini ya mtu mmoja kupewa mtu mwingine naona hayako poa kabisa. Waachane na huo utaratibu.

Yaani Hata wiki haijaisha kuna jamaa nilimpigia simu baada ya kutowasiliana naye kwa muda mrefu , nashangaa anapokea mdada. Namuuliza imekuwaje ananijibu hiyo laini anayo karibia miezi mitatu sasa. Na usajili ni wake hata ukiangalia kwenye huduma za kipesa.
 
Yaaah miezi mitatu...anapewa mwingine otherwise umetoa report kabla

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Cha ajabu ambacho huwa najiuliza bila kupata majibu:

Unapoenda kwa wakala, kuna namba(line) mpya maelfu zinazosubiri wateja!

Cha kushangaza, ukipokonywa namba huwezi kurenew tena kwa namna yoyote, maana huwa imeshauzwa!

Swali: namba wanazopokonywa clients huwa zina utamu gani kununuliwa ghafla kwa kasi ya upepo na huku namba mpya zikiwa zimerundikana bila usajili wa haraka?

Tunanunua namba kwa pesa na kumilikishwa kuwa ni mali yetu binafsi, wanapoipokonya bila fidia huo siyo uharamia na wizi?

Hawaoni kusajili kwa njia ya Nida na kisha kuporwa ni kuhadaa taarifa na falagha za watu?

Pia kuleta usumbufu mkubwa kwa anayeinunua namba ya zamani ya mtu mwingine kwa kuendelea kupokea simu zisizoeleweka kwa muda mrefu na usiojulijana?
 
Hayo ni miongoni mwa mambo ambayo TCRA wanapaswa wayatolee ufafanuzi wa kina kabisa.
Nafikiri TCRA na mitandao ya simu waweke namna ya mtu Kuhold namba yake kwa kutoa Taarifa moja kwa moja kutoka kwenye namba yake ya SIMU kwa Kuihifadhi kwa ajili ya Matumizi ya Baadae.Kiteknolojia linawezezekana
 
Ila kwa kweli haya mambo ya laini ya mtu mmoja kupewa mtu mwingine naona hayako poa kabisa. Waachane na huo utaratibu.

Yaani Hata wiki haijaisha kuna jamaa nilimpigia simu baada ya kutowasiliana naye kwa muda mrefu , nashangaa anapokea mdada. Namuuliza imekuwaje ananijibu hiyo laini anayo karibia miezi mitatu sasa. Na usajili ni wake hata ukiangalia kwenye huduma za kipesa.
Cha ajabu ambacho huwa najiuliza bila kupata majibu:

Unapoenda kwa wakala, kuna namba(line) mpya maelfu zinazosubiri wateja!

Cha kushangaza, ukipokonywa namba huwezi kurenew tena kwa namna yoyote, maana huwa imeshauzwa!

Swali: namba wanazopokonywa clients huwa zina utamu gani kununuliwa ghafla kwa kasi ya upepo na huku namba mpya zikiwa zimerundikana bila usajili wa haraka?

Tunanunua namba kwa pesa na kumilikishwa kuwa ni mali yetu binafsi, wanapoipokonya bila fidia huo siyo uharamia na wizi?

Hawaoni kusajili kwa njia ya Nida na kisha kuporwa ni kuhadaa taarifa na falagha za watu?

Pia kuleta usumbufu mkubwa kwa anayeinunua namba ya zamani ya mtu mwingine kwa kuendelea kupokea simu zisizoeleweka kwa muda mrefu na usiojulijana?
Nafikiri TCRA na mitandao ya simu waweke namna ya mtu Kuhold namba yake kwa kutoa Taarifa moja kwa moja kutoka kwenye namba yake ya SIMU kwa Kuihifadhi kwa ajili ya Matumizi ya Baadae.Kiteknolojia linawezezekana

Kwa bahati mbaya sana, kutokana na Visa vya uzoefu kuhusiana na masuala haya ya kubadilishwa kwa Wamiliki wa SIM Card za Simu, baadhi ya Maafisa wa Vyombo vya Usalama wasio waadilifu wamekuwa wakilitumia Jambo hili vibaya sana na kuhujumu vibaya Haki za watu. Naamini kwa dhati kabisa kwamba TCRA kwa namna moja ama nyingine watakuwa wanalijua suala hili na/au na wao pia ni sehemu mojawapo ya Wahusika wa kufanikisha missions za namna hiyo.

Kuna Visa na Mikasa mingi Sana ipo imejificha nyuma ya masuala haya ya kubadilisha na kuhamisha umiliki wa SIM Cards kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa Mtu mwingine.
1. TCRA wanapaswa wajitokeze hadharani ili walitolee Maelezo ya kina kabisa kuhusiana na masuala haya.
Sitaki kuingia kwa undani zaidi kwa sasa kuelezea suala hili kwa Sasa.

2. TCRA pia wanapaswa waweke Kanuni Mpya za Sheria zitakazomruhusu MMILIKI HALALI WA SIM CARD kuweza Kupata Taarifa zake Binafsi za Faragha za Matumizi ya Mawasiliano yake ya Kimtandao pale Mmiliki huyo Atakapozihitaji kutoka kwa Mtoa Huduma wake wa Mtandaoni wa Simu (Service Provider).
Mmiliki wa SIM Card awe na HAKI ya Kupata Taarifa ya Mwenendo wa Matumizi yake ya Simu aliyofanya kupitia kwenye Namba yake ya Simu ambayo anamiliki kihalali. Mathalani, Service Provider wa Mtandao wa Simu ampatie Mteja wake Print out ya Messages, Voice Notes, Rekodi za miamala ya Fedha kupitia kwenye Namba yake, etc.

Watoa Huduma za Kimtandao wanapaswa wafanye hivyo sawa sawa na vile ambavyo Benki za Biashara zinavyotoa Bank Statements kwa Wateja wao. Isiwe Mapolisi tu ndio wenye Haki za kuweza kupatiwa taarifa za namna hiyo.
 
Jambo hili linapaswa kutazamwa tena upya kutokana na unyeti wake.

Ni lazima kabisa Serikali kupitia TCRA iweke Wazi kabisa kuhusu HAKI na WAJIBU wa Wamiliki hao tofaufi wa SIM Card kuhusiana na masuala haya ya kubadilisha Mmiliki wa SIM Card za simu kwa sababu suala hili linahusisha Usalama wa Taifa. Tukumbuke kwamba, suala la Usalama wa Taifa zima linaanzia na Usalama wa mtu mmoja mmoja katika Jamii.
Uko sahihi.
Wao hawajali wanauza kifaa cha mawasiliano utadhani wanauza maandazi au madafu.
Hii ishu ina madhara makubwa sana maana yule mmiliki mpya wa Akaunti anaweza akawalaghai na kuwatapeli watu wako wakadhani ni wewe
 
Back
Top Bottom