Nimekutana na mwanamke wa ajabu, naanza kuingiwa na hofu walimwengu nisaidieni

Hii mbona ni ile nyimbo wa mheshimiwa temba ya side mnyamwezi!
 
Ngoja niseme kitu kidogo ili mwenye kuona aone.

Hivi mnafikiri ufalme wa shetani umefitinika?? Eti uumwe au upagawe na Mapepo halafu uende kwa mganga alitoe pepo wapi na wapi???

Ambacho waganga wanafanya kwa watu ni hiki. Anakupatia Pepo kubwa ambalo linakuja na kulitiisha au kulituliza lile dogo ulilonalo kwa hiyo wewe utaona kuwa tatizo limekwisha kumbe ndio una hali mbaya zaidi. Haya mambo ni ya kiroho na huwezi kugundua kitu. Ili uweze kumudu hili pepo nalo linakuja na masharti yake ambayo mganga anakupa. Ukiyashindwa au ukikiuka hayo masharti utakipata cha Moto kwani hali yako itakuwa mbaya zaidi.

Kitu pekee na suluhisho la kweli ni Mungu basii. Walipitia hayo au hata washirikina wanaosoma haya wanajua kama hii ni kweli.

Ufalme wa shentani haujawahi kufitinika. Kamwe Pepo hawezi kumtoa pepo mwenzake. Yesu alisema hivi.

Mathayo 12:24-28
[24]Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.
[25]Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.
[26]Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?
[27]Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.
[28]Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.

Kwa hiyo dawa ya hayo mapepo ni Roho wa Mungu pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…