Nimekuwa nikitafakari kuhusu Biblia na namna waandishi wake walivyoandika matukio mbalimbali kuhusu Yesu. Mambo kadhaa yananipa maswali

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
1. Biblia inasema Yesu alifunga kwa siku arobaini jangwani, akiwa peke yake, na akajaribiwa na Shetani. Nani alirekodi majaribu hayo wakati hakukuwa na mtu mwingine aliyeshuhudia na hakuna sehemu inayosema Yesu alisimulia tukio hilo?

2. Katika bustani ya Gethsemane, Yesu alienda kuomba kwa huzuni sana, huku wanafunzi wake wakilala pembeni. Kwa kuwa wanafunzi walikuwa wamelala, ni nani aliyesikia au kurekodi maombi hayo ya ndani aliyotoa kabla ya kusulubiwa?

3. Wakati Yesu alipojaribiwa na viongozi wa kidini, hakujitetea waziwazi au kueleza mengi kuhusu maandiko aliyoyafundisha. Kwa nini Yesu alichagua kukaa kimya badala ya kujitetea au kufafanua kwa undani zaidi?

Hebu tujadili na kufungua mawazo mapya kuhusu maswali haya yenye uzito wa kiimani na kihistoria.
 
Dini ni njia iliyotumika na wakoloni kututawala sisi waafrika kama Dini zilikuwepo zingekuja moja Kwa moja mpaka Africa
 
Mhh funga na kuomb Mung asem.na wwe [emoji2788][emoji2788][emoji2788][emoji18]
 
1. Biblia inasema Yesu alifunga kwa siku arobaini jangwani, akiwa peke yake, na akajaribiwa na Shetani. Nani alirekodi majaribu hayo wakati hakukuwa na mtu mwingine aliyeshuhudia na hakuna sehemu inayosema Yesu alisimulia tukio hilo?
Ukisoma Injili ya Yohana mwishoni kule inasema kabisa matukio ya Yesu yote yangeandikwa yasingetosha, alaf si unaelewa kwamba biblia imeandikwa na watu ambao wamekuwa inspired na roho mtakatifu, chukulia mfano wa jinsi yohana alivoandika ufunuo

3. Wakati Yesu alipojaribiwa na viongozi wa kidini, hakujitetea waziwazi au kueleza mengi kuhusu maandiko aliyoyafundisha. Kwa nini Yesu alichagua kukaa kimya badala ya kujitetea au kufafanua kwa undani zaidi?
Kukaa kimya was the best choice, unajiteteaje kwa watu ambao wapo radhi wamfungue jambazi atoke jela ili wamsulubishe mtu ambae hakufanya lolote zaidi ya kuponya wagonjwa na walemavu.
 
Leo ngoja nijaribu kujibu na mimi;

1. Majaribu ya Yesu Jangwani:
Ni kweli hakuna mtu aliyekuwepo kushuhudia majaribu ya Yesu jangwani. Biblia inasema kwamba Yesu alikuwa na Roho Mtakatifu (Luka 4:1)
"Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu,
alirudi kutoka Yordani, akaongozwa.
na Roho muda wa siku arobaini.
nyikani"

Inawezekana baada ya tukio hilo, Yesu alisimulia wanafunzi wake kilichotendeka, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, wakaandika katika injili. Biblia iliandikwa kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hata kama hakukuwa na shahidi wa kimwili, Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa injili kuandika ukweli kuhusu majaribu ya Yesu.

2. Katika bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwa sauti, inawezekana wanafunzi wake walisikia baadhi ya maneno yake japo walikuwa wamelala usingizi. Pia, tunaweza kusema kwamba Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa injili kuelewa uzito wa maombi ya Yesu na kuandika kiini chake.

3. Kuna sababu kadhaa zinazoweza kuelezea kwa nini Yesu alichagua kukaa kimya mbele ya wale viongozi:
Alitimiza unabii: Kimya chake kilitimiza unabii wa Isaya kuhusu Mwana-Kondoo wa Mungu atakayepelekwa kuchinjwa bila kufungua kinywa chake (Isaya 53:7)
"Alionewa, lakini alinyenyekea,
Wala hakufunua kinywa chake;
Kama mwana-kondoo apelekwaye.
machinjoni,
Na kama vile kondoo anyamazavyo
Mbele yao wakatao manyoya yake;
Naam, hakufunua kinywa chake."

Alionyesha ukuu wake: Yesu alijua kwamba hoja zozote asingetoa zisingewashawishi viongozi hao waliokuwa wamejaa chuki na wivu. Kimya chake kilionyesha ukuu wake juu ya shutuma zao za uongo. Alichagua kukaa kimya ili kutimiza kusudi lake kuu.
 
Watakuambia ni mambo ya rohoni , utapeli mtupu.
 
Leo ngoja nijaribu kujibu na mimi;

1. Majaribu ya Yesu Jangwani:
Ni kweli hakuna mtu aliyekuwepo kushuhudia majaribu ya Yesu jangwani. Biblia inasema kwamba Yesu alikuwa na Roho Mtakatifu (Luka 4:1)
"Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu,
alirudi kutoka Yordani, akaongozwa.
na Roho muda wa siku arobaini.
nyikani"

Inawezekana baada ya tukio hilo, Yesu alisimulia wanafunzi wake kilichotendeka, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, wakaandika katika injili. Biblia iliandikwa kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hata kama hakukuwa na shahidi wa kimwili, Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa injili kuandika ukweli kuhusu majaribu ya Yesu.

2. Katika bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwa sauti, inawezekana wanafunzi wake walisikia baadhi ya maneno yake japo walikuwa wamelala usingizi. Pia, tunaweza kusema kwamba Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa injili kuelewa uzito wa maombi ya Yesu na kuandika kiini chake.
Vipi aliyesema ametokewa na Jibrili pangoni?
 
Na vipi kuhusu Adam na demu wake Eva, Musa akiongea na Mungu kupitia kichaka cha moto, mtume Mohamad pangoni alikodai kashushiwa quran. Nani alikuwepo? ama Yesu ndie mnyonge wako? au kwakuwa Yesu ana mashabiki kibao unajua utatrend? mnachosha sana na issue za akina Yesu, kuna news kibao leo hii habari ya mjini, kuna Trump na Kamala, kuna mwamba Guinea kagonga wake za watu 400 mpaka ndugu zake wa damu.2 Hujaona kama mambo ya kujadiri?
 
Huwa najiuliza sana kwanini kadri siku zinavyozidi kwenda watu wengi wanapoteza sana imani juu ya uwepo wa MUNGU??
 
4. Kwanini watu wanataarifa za kutungwa mimba na kuzaliwa lakini hawana taarifa akiwa kijana mpaka anafikia miaka 30!
5. Kwanini azaliwe kwenye mavi ya ng'ombe kuliwa hakuna sehemu nyingine zaidi ya hiyo?
6. Kwanini mama yake ni bikra hata baada ya kuzaa watoto wengine kwa njia za kawaida?
 
1. Biblia inasema Yesu alifunga kwa siku arobaini jangwani, akiwa peke yake, na akajaribiwa na Shetani. Nani alirekodi majaribu hayo wakati hakukuwa na mtu mwingine aliyeshuhudia na hakuna sehemu inayosema Yesu alisimulia tukio hilo?

2. Katika bustani ya Gethsemane, Yesu alienda kuomba kwa huzuni sana, huku wanafunzi wake wakilala pembeni. Kwa kuwa wanafunzi walikuwa wamelala, ni nani aliyesikia au kurekodi maombi hayo ya ndani aliyotoa kabla ya kusulubiwa?

3. Wakati Yesu alipojaribiwa na viongozi wa kidini, hakujitetea waziwazi au kueleza mengi kuhusu maandiko aliyoyafundisha. Kwa nini Yesu alichagua kukaa kimya badala ya kujitetea au kufafanua kwa undani zaidi?

Hebu tujadili na kufungua mawazo mapya kuhusu maswali haya yenye uzito wa kiimani na kihistoria.
Nataka kujua basda ya Yesu kubarehe je nini aliona kuwa sasa amebarehe?

Pili je Yesu aliwahi kutongoza mwanamke?
Tatu je Yesu alitahiriwa.
 
Back
Top Bottom