Matrundanjariya
New Member
- Nov 30, 2024
- 1
- 3
Habari zenu Wana jamiiforums,
Ni mwenyeji wa mkoa wa Singida, naombeni connection ya kibarua iwe ni ujenzi (kama saidia fundi au kupanga pavings Nina uzoefu nayo) yaani chochote hata Cha kulima, kusafisha mashamba kwa maeneo ya huku Pwani ya kibaha maana Mimi nipo sehemu inaitwa mlandizi.
Sina chochote hivyo nataka nipate japo hela ya kula na sehemu ya kulala tu halafu nijipange kurudi mkoani, maana kwa Hali niliyonayo sina uwezo wa kurudi hivihivi na Niko na familia kule.
Safari yangu ya kuja huku ilitokana kuwasiliana na mwenyeji wangu ambaye kwa mujibu wa maelezo yake aliniambia anajishughulisha na ujenzi hivyo angenifanyia mpango wa kazi hizo afanyayo yeye, bahati mbaya nilipofika mawasiliano yalipotea yaani akawa haupatikani Sasa sijui kama alinizimia simu au alipatwa na Nini.
Hali hiyo imenifanya nijikute Niko gizani kabisa sijui Nini nifanye, nimejaribu kutembea saiti mbalimbali za ujenzi yaani ni kutembea tu nitakapopata kuna shughuli naulizia lakini nyingi unakuta watu wametimia ngumu kupata nafasi. Imekuwa ni kubahatisha sana nafikiri pia ugeni wangu unachangia.
Kuna msemo wa kuwa kimsaidiacho mtu chake nilijaribu labda niuze simu yangu inisaidie lakini thamani yake ikawa ni ndogo sana nikipiga mahesabu haiwezi nisaidia bali itaniongezea shida nyingine ya kukosa mawasiliano.
Kwa yeyote mwenye kuguswa kunisaidia shughuli au ushauri nitashukuru.
Mungu awabariki.