Roho nyepesi ndo ulie hata vya uongo?...mimi roho yangu nyepesi lizzy...
ulivopewa ban wewe hujalia?
pole sana
karibu tena love
acha tu bro watu sio watu siku hizi wanathamini sana hela aisee ,huyu hata akiambiwa aue mtoto si anaua?maneo ya mkosaji hayo
Ngepata hiyo buku na mia tano ungepewa sifa mpaka basi
Sasa kakosa alichotaka anaona bora akutukane
Na aahh (samahani lakini) nilijua ameanza kukutupia nondo uwe mke wake kumbe ni hayo
Achana nae bana wala asingekuharibia siku
Ulipaswa udharau na uendelee na mambo yako
My sweet wifi Cantalisia mie good mwaya, vipi wewe na my bro mwaendeleaje?..Darling Wifi mzima weye?
Huyu mbabu hakujua Smile roho yake nyepesi lol!
Sijui ni mfanyeje huyu mzee jamani?
Huu ni uungwana?
Huu ni utu?
ngoja nilale kidogo ......
tena nasikia ni baba mdogo yake rejao ndo kampa na tishertPole sana mwaya japo nimecheka mpaka basi lol!
Huyo mbabu hana lolote njaa tu ndio ilikua inamsumbua,
Ungemwelewa mapema wala usingepoteza machozi yako kwa mtu alokosa ustarabu km huyo!!
umeona eeehuklichokua unalia ni kipi kati ya hivi
Mzee kula lit sheti la magamba wakati serikali inataka kuvunja baraza
au mzee kubwabwaja ujinga mwingi kama vile anakufahamu sana au
mzee kuomba hela bila aibu yeyete wakati amevaa gwanda hata mimi
ungekua umempa hela hata shilingi na mimi ningeongeza tusi
ila we ni mjanaj acha ale jeuri yake hao ndio wanauzaga kura zao halafu
wezi wanakula hadi fedha za maendeleo yao wanaanza kuomba?
pole sana...........................
My swty Wifi sweetlady Smile anaonekana na heshima sana na hawajui hawa wababu wakiwa na njaa wanashukaga vesi za ajabu,My sweet wifi Cantalisia mie good mwaya, vipi wewe na my bro mwaendeleaje?..
Huyu Smile hawajui wazee wa kijijini vizuri ndio mana akalia lol. Kwanza namshangaa kumpa nafasi huyo mzee ya kusema maneno yote hayo. Muulize husband wako Rejao manake anawajua vema wa pale kijijini kwetu...
Hahaha hahah hahah,tena nasikia ni baba mdogo yake rejao ndo kampa na tishert
utakoma
labda umpe atm card yako
wakwe hao
Hapo ndio patamu coz ni aibu kuomba hela huku anaongea kiinglish,mbona kiinglishi wanajua? utakoma nakwambia
sikuwa na hata hamsini.... mwenzenuHuyo mzee hazimtoshi. Mara ngapi tunakutana nao mitaani, anakulenga kirungu ukimkatalia anaporomosha ya kuporomosha. Kama ni mimi wala nisingekasirika; baada ya kumwaga malusinde yake, ningempa hiyo elfu moja au mbili, nione angegeuza upande upi wa santuri.
Angeendelea.....
Watoto wa siku hizi bwana, hamtaniwi.
Mimi na babu yako tulikuwa tunataniana sana,
na kasoro kidogo niwe mume wa nanihuyu wako,
lakini naniyule wako akanizidi ujanja. Mi nilijua tu
huwezi kumnyima babu yako pesa ya dagaa.
Sasa vipi, utapita nyumbani baadaye uje kuonana
na bibi yako? Blah blah blah!
Hapo ulijikosesha senema ya bure.
Nnachompendea kakangu Rejao ni vile amejitahidi kukupa tahadhari zote kabla ya hatari lol....wifi nifikishie salam kwa kaka!