A
Anonymous
Guest
Wana JF salama humu ndani, mimi ni mwanachama wa siku nyingi lakini ni nadra kuniona nikitumia jukwaa hili la Fichua Uovu, nimeona malalamiko mengi yanayowekwa huku yanafanyiwa kazi na mamlaka, nikaona sio mbaya nami nikifikisha hili langu kwa njia hii ili lifike mbali zaidi.
Sisi wakazi wa Mwanza naomba mtusaidie kupaza sauti kwa changamoto tunayopitia kwa hawa ndugu zetu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) upande wa Mwanza!
Niliwalipia wategemezi wangu watatu (Watoto 2 na mama yao) kiasi cha shilingi 432,000 tarehe 22/08/2023, nikaambiwa baada ya mwezi nikachukue kadi!
Nikaenda baada ya mwezi nikaambiwa “bado”, niende baada ya wiki moja, nikaenda nikaambiwa “bado, njoo baada ya wiki”.
Umefika huo muda nilioambiwa mara ya mwisho naambiwa “bado” (naandika haya nikiwa na hasira sana).
Bahati mbaya mtoto akaugua nikaenda kuomba kibali cha kutibiwa nikaambiwa nisubiri, hadi leo siku ya tatu bado hakuna lolote!
Sijui tatizo ni uwajibikaji au ni nini maana pale Ofisi ya NHIF Mwanza wenye matatizo kama haya ni wengi sana na hakuna pa kusemea, ukibishana nao wanakuitia Mgambo na hela yako wameshachukua!
Risiti ya malipo ipo na hakuna cha kuwafanya NHIF, ninayeteseka na kuumia ni mimi na familia yangu.
Pia soma: Tabia ya NHIF Tabora kuchelewesha kadi za Bima za Uanachama inatuumiza wengi