Nimemchoka huyu mrembo wa chuo kikuu

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,635
Reaction score
4,160
[emoji121]
WAKUU,

HAPA #UBUNGO_MSEWE NILIPOPANGA HIKI CHUMBA CHANGU CHA UANI AMBACHO NALIPIA KODI TASLIMU YA SH. 11,500/= KWA MWEZI
NA NIMELIPIA KODI YA MUDA MREFU YA MIEZI MITATU-
CHUMBA CHA PILI KAPANGA BINTI MWANACHUO.

HUYU BINTI NI PINI MATATA SANA MWENYE SURA NA FIGA MAPACHA KABISA NA #Hamisa_Mobeto.

KUTOKANA NA UBIZE NILIOKUWA NAO KWENYE MISHEMISHE ZANGU ZA KUBEBA TOFALI KULE PANDE ZA KIMARA BUCHA,
HUWA NAPUMZIKA WIKENDI NA USIKU TU!

------------
SASA KAMA KAWAIDA YANGU KILA NAPOTOKA KWENYE MISHEMISHE ZANGU JIONI HUWA SIPOTEZI MUDA,

NAWASHA JIKO LANGU LA KUNI
NAPIKA UGALI WA DONA ½ KILO,
KISHA NAUACHA KWENYE SAHANI YANGU YA KUBWA YA BATI BILA KUUFUNIKA ILI UPOE NA UWE MGUMU KAMA TUFE LA KWENYE UMISETA(ili nishibe),

WAKATI HUO NIKIPIKA MBOGA YA DAGAA KAUZU WA KUKAANGWA BILA NYANYA (maana'ke nyanya zimepanda bei balaaaah huku kitaa).
****
SASA KITU KINACHOBOA
HUYU MREMBO MWANACHUO KAANZA KUNIZOEAZOEA
NA HUWA HACHEZI MBALI PINDI NAPOPIKA 'Ndumbi' LANGU MATATA.

ANAKUJA NA TEKNIKI YA KUNIULIZIA BEI YA TOFALI,
HALAFU KILA SIKU USIKU ANANIPIGISHA STORI MBALIMBALI
HASA MIDA YA UGALI,
NA NIKIMKARIBISHA-
HAACHI KITU,
PAMOJA NA KUWA UGALI UMEKOMAA KAMA TUFE LA UMITASHUMTA
BINTI ANADUFUA MPAKA MWISHO NA KUOSHA VYOMBO KABISA!

KISHA NAPOMUAGA KWENDA KULALA,
KWA SAUTI YA MAHABA, KUREMBUA NA KUNENG'ENEKA
ANASEMA,

"Nice of you @Seneta_Wa_Mtwiz,
You better quit the toiling job you're doing,
And be a chef,
Because you are so good at cooking &
I would be very pleased.

Take it from me."

---------
SASA WAKUU,
HIVI LEO NIKIMCHENJIA NIKAMWAMBIA HAKUNA KULA UGALI WANGU MPAKA
ATOE MCHANGO WA KUNUNUA UNGA NITAKUWA NIMEKOSEA WAKUU?

MAANA'KE NIMEMCHOKA SASA,
HII NI WIKI YA PILI MFULULIZO ANADOEA MENYU YANGU,
MTWARA TUNASEMA "anakopoka!"

[emoji121] [emoji121] [emoji121]
[emoji121] [emoji121] [emoji121]
 
kayapenda mapishi yako mkaribishe kila siku acha uchoyo boom lenyewe halimtoshi
 
Mbeba tofali unapata wapi muda wa kuwa online na kuchat, Wachaga unawajua kweli ? Anawezaje kukuruhusu uchati bBadala ya kumwagilia tofali maji.
 
Hapo jikotee tu... Usishangaa akakuajiri uwe mpishi wake... All ze best ila usiache kuwa na Dawa ya penzi chumbani...
 
mkuu wee vumilia tuu ukiona ivo ujue kuna kitu kitamu zaidi ya ugali kinakuja vuta subra

Relax alaf hema hema kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…