Jana mke wangu amewapeleka watoto wetu pale Aga Khan walk kucheza skating. Mwanangu wa kiume akapata ajali mbaya iliyomfanya ang'oke meno tatu, wakati anafanyiwa huduma ya kwanza, jamaa fulani kawapigia Sonko rescue team and baada dakika chache ambulance yao ikafika na kumpeleka hospitali.
Kwa kweli mimi huwa sijamkubali Sonko na vituko vyake, lakini jana nilihisi tofauti. By the time nafika hospitalini kuungana na jamii yangu, tayari mtoto alikua amefanyiwa matibabu. Hapakua na muda kuwaita AMREF ambao huwa nimejiunga na huduma zao.