Nimemkumbuka marehemu Raphael Paul RP na Twaha Hamidu 'Noriega'

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kuna watu wajinga sana, wengine sisi tumeanza kwenda uwanja mwaka 1988 enzi hizo wengine hamjulikani kama mtazaliwa, eti sijamuona Roster Ndunguru nimesimuliwa, mimi niliyezaliwa Ocean Road nisimjue marehemu Roster Ndunguru, Muhiddin Pazi nisimjue, Abbas Kuka? John Bosco nyie wehu kweli.

Haya sasa Leo nimemkumbuka marehemu Raphael Paul na Twaha Hamidu Noriega.Katika mabeki wa kulia wa Simba niliowahi kuwashuhudia huyu RP alikuwa hana mfanowe kwangu, nimewaona akina Abubakary Kombo, Deo Mkuki, Rashid Abdallad, Sylvanus Ibrahim Polisi akitoka Yanga, Mavumbi Omary, Somebody Kazimoto kutoka Ushirika Moshi, Said Sued, Barbara's Sekelo, Ndandou Ramadhan akitokea Yanga, Kasongo Athuman na wengineo nimewasahau lkn RP alikuwa habari nyingine, ni mfupi na mnene lakini alikuwa anajua kumwaga maji.Akianzishiwa tu kipa Mosses Mkandawile spidi yake ni supersonic.

Huko kushoto Twaha Hamidu naye alikuwa kiboko, walikuja akina Alphonce Modest, siku nyingine anacheza Deo Mkuki akitokea Pamba, Ramadhan Watso lkn Noriega alikuwa mtu na nusu.Mungu akupe afya Twaha Hamidu Noriega.

Nawakumbuka sana wewe na mshambuliaji Malota Soma Ball Juggler, natafuta zawadi niwapatie, burudani mliyonipa enzi za utoto wakati nawaangalia hazipo tena, sijui Lomalisa sijui nani.Kha.
 
Umezaliwa 1979 Kwa hiyo 1988 ulikuwa na miaka 9 usitusumbue.
 
Class mate fikiri magoso
 
Sasa huyu Lomalisa ni beki wa Simba? Kwanini ulivyoanza na usimba wako usimalize hadi mwisho na usimba wako. Huyu Lomalisa anakuhusu nini wewe badala ya kulinganisha hao mabeki uliyowakumbuka na mabeki wako wa sasa wa Simba
 
RP jamaa alikuwa mpole sana ila kipisi cha mtu alifanana na Thobias Nkoma.
 
Kuna watu wamezaliwa miaka 1988 hapo hapo ocean road na wao waliwaona hao akina Noriega?kigezo ni kuzaliwa ocean road acha uzwazwa.
 
Sasa huyu Lomalisa ni beki wa Simba? Kwanini ulivyoanza na usimba wako usimalize hadi mwisho na usimba wako. Huyu Lomalisa anakuhusu nini wewe badala ya kulinganisha hao mabeki uliyowakumbuka na mabeki wako wa sasa wa Simba
Huyu jamaa ni hoho
 

"We will play football together in heaven,'​

says Pele in tribute to Diego Maradona​


Walale Pema huko Mbinguni.
 
Kuna watu wamezaliwa miaka 1988 hapo hapo ocean road na wao waliwaona hao akina Noriega?kigezo ni kuzaliwa ocean road acha uzwazwa.
1988 ocean road haikuwa maternity, miaka ya 70's aliyezaliwa Dar maternity ilikuwa ni ocean road.

Ukisikia mtu anakwambia amezaliwa Muhimbili miaka ya 70's huyo ni muongozo, maternity ilikuwa ni ocean road.
 
Hapa umetaja majina ya wachezaji wa Simba tu, hapo wengi hawacheza pamoja.

Ni sawa umtaje Okwi na Baleke kuna gap kubwa hapo.
 
Twaha Hamidu alianza Kama mshambuliaji namba 11 baadae akabadilishwa kuwa beki. Alikuwa na mapafu ya mbwa.
Raphael Paul alianzia pamba baadae akahamia Simba alikuwa Aina ya mabeki wanaozuia na kupanda. Hakujua kucheza rafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…