sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,182
- 8,948
Asubuh ya leo mnisamehe nimemkumbuka. Rafiki yangu Afande Mashaka aliyekufa kifo kibaya zaidi ya miaka takribani kumi iliyopita.
Nakumbuka Mimi nilikuwa kidato Cha sita hapo Azaboy, ndipo nilipo pewa taarifa yakuwa Afande Mashaka anaumwa sana na yupo kota za police Pale Obey, enzi hizo kulikuwa na kota za bati kama mabanda ya kufungia kuku sijui kama yapo mpaka leo ila kama yapo basi naomba yasibomolewe yabakie kama majumba ya makumbusho Ili Kila nikija dar nifike nifanye tambiko la kuapa kutenda haki maana Rafiki yangu Mashaka alikuwa Afande hasiye Tenda haki na Sasa ni Marehemu Afande aliyekuwa hatendeki haki.
Baada ya kupata taarifa nilifika pale kota, na kumkuta rafiki yangu Afande Mashaka akiwa anatokwa na Damu Kila sehemu yenye uwazi kwenye Mwili wake,ndugu yangu usiombe ukutane na karma ya namna hii jamaa alikuwa anaumwa na kichwa Kila kilipomgonga akitokwa na Damu kila pahala Yani mpaka sehemu ya haha ndogo na kubwa puani,kwenye vinyweleo kote kulitoa Damu.
Baada ya kufika kwake pale kota jamaa alifungua mdomo na kuniambia Rafiki yangu Sifileo Mimi leo nakufa ila nakwambia kabsa chanzo Cha kifo changu ni uonevu nilio ufanya sijui ni kwa padri au mpemba ila alikuja bwana mmoja amevaa Kanzu pale kwenye ATM ya crdb Namanga.
Kwa msio jua au vitoto vya siku hizi mnao vamia Jiji ambalo tulikulia sisi mataikuni wa mjini,yaani Mimi Sifi leo, kassimu Suna na kandyamwoyo, Namanga ni jina la sehemu liliopo msasani pale Makangira, ni karbu sana na kituo Cha polisi obey hapo.
Uwezi amini baba zamani iliwai tokea jambazi alikuja kuiba pale Namanga Bureau D change, akapiga tukio pale akaiba mamilioni akamaliza akaingia buchani pale akanunua nyama, akapaki kwa gari akapitia katikati ya kituo Cha polisi obey na Ubalozi wa marekani na kusepa kusiko julikana huku akipga risasi juu hakuna askari hata wa dawa alikuwa pale kituoni yaani Enzi za Mahita Bwana hacheni bwana,Yani jina Mahita halikufaa kubakia humo jeshini niliumia nilipo sikia Ana mtoto Tena mwenye cheo kikubwa jeshi la polisi sijui ni yule aliye mzaa na house girl wake mie sijui.
Niendelee na story bhana ya Namanga ni Mengi;
Basi Mashaka alinisimulia yakuwa Akiwa lindoni alikuja bwana mmoja kuchukua pesa kwenye ATM yeye kama Asakri wa zamu alimuona yule bwana akiwa amevalia Kanzu nyeupe, akiingia ndani ya kijiofisi Cha ATM na kumkuta yeye Afande. Mashaka ndani akiwa ameshika mtu wa bunduki, basi alimpisha yeye akatoka nje kidgo,yule mvaa Kanzu aliingia na kuingiza ATM Kasi kwenye mashine na kutoa kiasi kisicho pungua milioni kadhaaa.
Tamaa yamponza.
Afande Mashaka kwa tamaa baada ya kushuhudia mvaa Kanzu akiwa na mablongoti ya pesa alimvamia yule bwana mule mule kwenye Kiofisi na kumpiga ROBA moja matata.na kumnyanganya zile pesa zote na kumtaka akimwachia aende akapande gar yake na kuondoka maeneo Yale haraka na paspo kupiga kelele,na endapo atapiga kelele atamfyatua kwa risasi.
Mvaa Kanzu alitoka nje huku akihema hasiamini kilichotokea jicho lishakuwa jekundu, yaani hapa nikwambie kitu msomaji wangu fanya zoezi kaka/dada usipo fanya zoezi inaweza tokea mtu akupige NGITA kidgo tu Yani mpaka ukajinyea ghafla.
Yule mvaa Kanzu aja ndogo ilimtoka,ghafla kwa mujibu wa Afande Mashaka, baada ya tukio lire yule mvaa Kanzu alikimbilia kwenye gari yake na kuwasha gar na kukimbia mithili ya mfungwa aliye achiwa kwa msaada wa Raisi aise.
Basi Afande Mashaka alikaa pale rindoni na burungutu la hela mfukoni mpaka walipokuja kumtoa rindoni majira ya saa kumi na moja na nusu,akapitia kwa demu wake mmoja alikuwa anaishi Namanga pale pale wakaanza kunywa moja moto moja baridi bar moja iliitwa Step In pale pale kwa wajuvi wa Dar enzi hizo mtakuwa mnapajua vyema.
Hayakupita hata massa mawili,Mashaka akianza kuishi maumivu ya kichwa na kufikishwa Namanga Dispensary pale, aise ndani ya dakika Tano baada ya pale jamaa alianza kutokuwa na Damu Kila pahala penye kitobo.
Akaamushiwa mwananyamala wanapima ugonjwa haunekani,baadae muhimbili Nako ugonjwa haunekani kabisa, baadae akashauriwa apelekwe Dodoma kwa bake mdogo dhen apelekwe Kijijini kwao kagera huko,akiwa njiani anampelekea Dodoma umauti ulimfika na kumwachia demu wake aliyejulikana kwa jina Tuse nae Sasa nilisikia ni marehemu ila nilisoma nae shule ya msingi Mbuyuni R.I.P my school mate wangu TUSE.
Baada ya kifo naazishi yaliyofanyika sijui Dodoma au kagera,habari zikaanza kusambaza mara alimpiga ROBA padri mara Mpemba kwa kweli haijawai eleweka ila yeye aliniambia alimpiga ROBA mtu aliyevalia Kanzu hakujua kama ni padri au ni Mpemba maana pale Namanga wapemba walikuwa wengi sana .
Kabla ya kupangiwa LINDO la ATM yeye alipewa kazi maalumu ya kuhakikisha anakamata vijana wote walio kuwa wanauza CD za ngono pale Namanga na aliwasafisha kisawasawa ila hakufanikiwa kumaliza maana Bado wapo mpaka leo wakina maneno na wengine(jina bandia).
Aliniuz sana kuwa kamata hao vijana enzi hizo maana wateja wao walikuwa ni Madoni wengine viongozi wakubwa wa kisiasa.sambamba na hayo pia Afande Mashaka alikuwa mtemi sana mwisho wake aliishia kabulini akiwa kijana mdogo sana hata mbegu hakuacha
Funzo; Askari polisi hacheni kuonea watu.ingawa sio Asakri wote wengine mu Wana wema.