Nimemkuta yu mjamzito!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu tuchukulie kwamba umekwenda kusoma nje ya nchi, au umekwenda mbali sana na nyumbani kwako kikazi. Umekaa huko kwa miaka miwili . unaporudi, unakuta mkeo ni mjamzito! Hebu niambie ungefanya kitu gani?
 
Mi nilijilipua juu kwa juu kabla hata sijarudi. Inauma sana! But the inshu hutegemea sana na jinsi mawasiliano, jinsi unavyomhandle, unavyompa majamboz ingawa hayo nayo ni relative terms.
 
Msamehe tu,kwani wewe huko hukumega?tofauti tu ni kwamba yeye kapata mimba.Msamehe msonge mbele
 
Msamehe tu,kwani wewe huko hukumega?tofauti tu ni kwamba yeye kapata mimba.Msamehe msonge mbele

Kweli amsamehe tu na washirikiane kumlea huyo mtoto wao mtarajia. Huo ndo uanaume wa kweli.
 
Unajua ukitaka kumukumu mwenzako jiulize kwanza wewe binafsi maisha yako hujawahi kucheat?then from there chukua hatua.akizaa na wewe weka mimba haraka kupunguza maumivu
 
hapana.......kama ningekuwa mwanaume......basi ningekuwa na uanaume wa uongo kwa hili......haifai

Wewe huoni wadada wenzio wanavyoshadadia eti jamaa amsamehe…..na ukisoma ndani, nje, pamoja na katikati ya mstari utagundua kwamba hiyo kauli yangu ni kejeli (sarcasm).
 
Hebu tuchukulie kwamba umekwenda kusoma nje ya nchi, au umekwenda mbali sana na nyumbani kwako kikazi. Umekaa huko kwa miaka miwili . unaporudi, unakuta mkeo ni mjamzito! Hebu niambie ungefanya kitu gani?

Ningemwambia Hongera mke wangu,i wish tutampata kidume!
 
Mhhh hapo hakuna kitu ni talaka tuu
Kwanza huyo mwanamke ana guts za kuendelea kunisubiri mpaka nije nimkute na hicho kitumbo.
Hata kama nje nilichakachua ila sikuleta huko mtoto
Sasa yeye anakula mpaka anashiba na kibend juu
 
hapa hakuna mjadara ni kufukuza hata kama unampenda kivi aende alikopenda zaidi
 
Kisukari wacha tuu. Hiyo ni balaa. Yaani hapo wala hakizungumziki kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…