Nimemnunulia mtoto Miwani lakini kavaa wiki tu lakini leo hii imetanuka

Nimemnunulia mtoto Miwani lakini kavaa wiki tu lakini leo hii imetanuka

Pelly

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
197
Reaction score
207
Habari zenu,

Naomba kuuliza kama kuna kuna anayejua shida hii ya miwani

Nimemnunulia mtoto MIWANI lakini kavaa wiki tu leo hii Anavaa umekuwa kubwa yaani inamvuka has wa akiinama., nitumie njia gani iweze kukaa vizuri bila kuvuka?

20250108_232812.jpg
 
Kawaone ma optometric Technician watampima na kuifahamu size ya fuvu lake na wata mtafutia frem inayomtosha.
 
Kuna kamba za miwani, ama kammbadilishie hiyo frem
Wengine wanafunga uzi na kuujaza eneo la kushikia mashikioni inabana haivuki ila kamba muhimu, mimi niliwahi tumia miwani miezi 6 tu nikiwa mtoto
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza kama kuna kuna anayejua shida hii ya miwani

Nimemnunulia mtoto MIWANI lakini kavaa wiki tu leo hii Anavaa umekuwa kubwa yaani inamvuka has wa akiinama., nitumie njia gani iweze kukaa vizuri bila kuvuka?

View attachment 3196269
Naona Biblia kwa mbaliiiii ... Mungu amponye mwanao apate kuona vema pasi na miwani
 
Why mtoto kununuliwa miwani?
Ana shida ya macho?
Nadhani kadri inavyowezekana hakuna ulazima wa mtoto kuanza kuvaa miwani kwa usalama wa macho yake.
Lakini hayo ni mawazo yangu!
 
Jf tunaonewa saana!
JF ni familia, Na katika familia hakishindikani kitu.

Tayari ufumbuzi umepatikana kulingna na michango ya wanafamilia wa JF.

Kheri ya waka 2025 MwanaFamilia wa JF
 
tatizo umenunua miwani bila kumpima mtoto au ulikuwa na vipimo visivyo sahihi..kwani kuna wenye kichwa chembamba kirefu,wenye kipana,wenye kichwa duara hivyo sio kila aina ya miwani kuvaliwa na yeyote..kwa ishu ya mtoto wako badilisha tu frame za miwani zitakuwa hadi mkunjo wa frame zimevuka masikio
 
Dah Mungu amsaidie dogo ila miwani ilichokuja kunifanya salaleeeee kama kuna dawa mpatieni tu dogo
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza kama kuna kuna anayejua shida hii ya miwani

Nimemnunulia mtoto MIWANI lakini kavaa wiki tu leo hii Anavaa umekuwa kubwa yaani inamvuka has wa akiinama., nitumie njia gani iweze kukaa vizuri bila kuvuka?

View attachment 3196269
Pole sana.
Iwapo mwanzoni miwani hiyo ilikuwa inamtosha, basi itakuwa imepanuka kwa sababu ya namna ya kuivaa na kuivua.
Inawezekana kuirejesha kawaida ikamwenea, lakini kunahitajika ujuzi kuirekebisha..

View: https://youtube.com/watch?v=oq2f_dl_aGs&si=mUBrh6FsDCrikzAp
 
Back
Top Bottom