kama ni hivi mlipie basi mahari halafu mwache akae kwao uwe unazaa naye tu mpaka upate idadi kamili ya watoto unaohitajiNachelea kusema ni mtoto wa nje ya ndoa kwani bado sijaoa. Nawaza kutooa kabisa ili nisiwe na mke niseyekuwa na furaha naye na pia nisiwe na watoto wenye mama tofauti tofauti
kama ni hivi mlipie basi mahari halafu mwache akae kwao uwe unazaa naye tu mpaka upate idadi kamili ya watoto unaohitaji
lakini jamaa hampendi....raha ya ndoa kupendana.....mapenzi ya kuoneana huruma hayafai....
kaka mwenye thread.....nakushauri fuata moyo wako.....
habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi Univeversity) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.
Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia hama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.
Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.
Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?
Kama hukumpenda mbona "uboho"wako ulisimama?na ukamuingizia mpaka kapata mimba binti wa watu?Kwani ukipanda korosho unatarajia kuvuna nn?au unataka kumtema kiaina?habari!
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 34, ni mwanafunzi wa Masters katika chuo kimoja hapa nchini. Nimehitimu chuo kikuu UCLAS (kwa sasa Ardhi Univeversity) mwaka 2008.Wakati nipo chuoni mwaka wa kwanza nilitokea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzangu,mahusiano ambayo mwanzoni sikuona kama yangefika mbali kwani hata jinsi yalivyoanza ilikuwa katika mazingira ambayo hakuna hata mmoja wetu aliyetarajia.
Tulihitimu chuo mwaka 2008 bahati nzuri kila mmoja wetu akapata kazi ingawa ni mikoa tofauti. Mara kadhaa nilimwambia umuhimu wa kuachana kwani nilihisi kuwa sitakuwa na furaha katika familia hama tutaoana lakini alipinga na kulia sana akidai kuwa yeye ananipenda sana. Nakumbuka wakati tuko chuoni alitaka hata kuacha chuo kwasababu yangu. Sikuwa tayari kuona hili linatokea hivyo niliendelea na mahusiano naye nikitafuta namna nitakavyoachana naye kwa amani.
Tuliendelea na mahusiano hayo ingawa sikuwa na furaha nayo na bahati mbaya niseme mwezi februari mwaka huu amenambia ana ujauzito wangu. Sifikirii kabisa suala la yeye kutoa mimba kwani kwa umri wangu nataka kuwa na mtoto. Nakumbuka katika mahusiano yetu sikuwahi kuishi naye kama mke wangu mtarajiwa hivyo mambo ninayopenda mke wangu awe nayo na tabia ninazopenda wala sikumuhimiza ayafanye.
Naomba ushauri nifanyeje nimechanganyikiwa, sitaki kuwa na watoto wa mama tofauti tofauti na pia nataka sana mtoto wake azaliwe salama?
Acha utoto mdogo wangu, cha kufanya badili mawazo yako jitahidi na kumwomba Mungu akusaidie ili uanze kumpenda huyo dada mfunge ndoa na kuanza maisha ya pamoja kama mke na mume na kulea mtoto wenu. Natamani sana ningeonana na wewe nikakushauri sana. Kwa sababu unaposema humpendi lakini bado ulikuwa radhi kufanya naye ngono mpaka kumpa ujauzito, nadhani kuna tatizo moja tu kuna vitu au tabia unataka awe navyo ambavyo nafikiri ukimkubali utakuwa umetatua tatizo kubwa sana kwani hutaona tena mapungufu aliyo nayo kama unavyoona sasa. Kitu cha msingi ni kwamba yeye ni mwanadamu, tena mwanamke na wewe ni mwanaume. Kwa hiyo, huo ndio msingi (au katika falsafa yaani philosophy tunaita substance) hayo mengine ya mvuto, tabia, na mengine ni accidentals ambazo zingine zinaweza kujengwa kwa mazoea tu.Nachelea kusema ni mtoto wa nje ya ndoa kwani bado sijaoa.
Nawaza kutooa kabisa ili nisiwe na mke niseyekuwa na furaha naye na pia nisiwe na watoto wenye mama tofauti tofauti
haukuwahi kusikia matangazo ya kutumia kifudusi(condoms)??????????