Nimempambania kapata kazi, salary ni 1.5m gross kaikataa kisa kapangiwa kwenda mkoani Mbeya

Mimi niliachaga haya mambo ya kuwatafutia watu kazi baada ya mpuuzi mmoja kuacha kazi Kigoma ili awe anashinda pale klabuni Yanga. Dogo alikua kwao ni Kigogo ila kila siku lazima aende pale klabuni Yanga kupiga stori. Mahaba yake na Yanga yakasababisha aache kazi.
 
Mwache tu hapo kwako, ni ndugu yako, wala msimsemeshe kuhusu hilo. Ana mipango yake, usimsakame.

Akikuwa ataacha.
 
Huyo umalaya unamsumbua. Anaogopa kumwacha mpenzi wake. Ana akili ndogo za kuona mbali. Siku kibarua kikiota nyasi na mpenzi wake amwambie kuwa ni mjamzito atakuomba tena umpiganie. Hapo ndipo unatakiwa umfukuze kama mbwa akili zimrudie
Hahahahahaha wengi wanaokataaga kwenda mbali huwa wanaogopa kuwaacha wapenzi wao.

Na ubaya akimwambia hilo mpenzi wake akiamini ni upendo, huyo mpenzi wake atamuona ni lofa wa kimataifa.
 
mfukuze akapange aone thamani ya 1.5. usimdekeze huyo. kuna nini anang'ang'ania dsm, au ana bwanake anaogopa wataachana?
 
Mwambie akatafute kazi ya dream yake.

Kikubwa umeshamsaidia vya kutosha. Itoshe umpe uhuru wake akasake kazi anaypipenda
 
Kwanza kabla ya yote, wape taarifa wazazi wake ili wasije kukulaumu kua umemfukuza ndunguyo, Kisha amka asbh siku moja tulivu kabisa, mpeakavu mabaya kabisa nape masaa ya kuondoka hapo usimuone tena
 
Duh.! Lakini mkuu usiache kusaidia wengine kwa sababu ya uzembe wa mtu mmoja tupo wengi wenye uhitaji wa ajira
 
Naomba msaada wako na Mimi huko viwandani kwa wachina tafadhari Kama bado una connection Hali ngumu hapa mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…