Ndugu zanguni, nimemsikiliza Mh. alipokuwa akiwahutubia Wana Diaspora Marekani. Moja kati ya masuala aliyozungumzia ni Katiba mpya. Nilichotambua ni kwamba, kama tutatembea kwenye mawazo yake, Katiba mpya haitapatikana leo wala kesho. Labda kizazi kingine huko mbeleni.
Kwa sababu kila anapozunguza anasema tuvute subira. Kama ni kuvuta subira tumeshavuta sana tena sana.
Majibu ambayo yalitakiwa yajibiwe na Serikali kuhusu utaratibu na muda wa kuleta Katiba mpya, anayajibu yeye.
Yaani, anaitetea Serikali kwamba haiwezi kuanzisha mchakato wa haraka ili kuharakisha upatikanaji wa Katiba mpya. Mbowe hata akiambiwa Katiba mpya hadi 2040, yupo tayari.
Kama wanaweza kuhujumu mali za umma haraka haraka, kusaini mikataba ya ovyo haraka haraka, kuchukua tozo haraka haraka, wanashindwaje kuanzisha mchakato wa haraka haraka wa kuleta Katiba mpya?
Ifahamike kuwa, CHADEMA ndo walioshika Bendera ya Katiba mpya, lakini nyuma yao kuna Watanzania wengi sana wanaopenda mchakato wa haraka haraka wa kuleta Katiba mpya.
Serikali inahitaji Pressure ya hali ya juu sana ili iweze kukubali matakwa ya Wananchi.
Kwa hiyo, mimi naungana na J. Heche, T. Lissu na wengineo katika suala hili la Katiba mpya.