Unaona iulivyo mpuuzi?
Kwa hiyo huwezi kutoa mfano hata mmoja, lakini unataka Tanzania isilinganishwe na nchi yoyote? Hiyo Tanzania ipo sayari ya pekee ambako matatizo yanayowapata wengine yenyewe haiyapati?
Hizo "NB" hazina maana yoyote kama huwezi kujibu swala la msingi.
Teh, teh, teh naona unataka kuniingiza kwenye siasa za viroja, kejeli, matusi na taarabu lakini huko siwezi kuingia. Hivyo wewe endelea kurusha vijembe lakini mimi nitakujibu tu hoja iliyoko mezani. Haya twende taratibu basi:
Mosi, Ujamaa nchini Tanzania ulifeli vibaya mno, hilo la kukimbilia kusema hata nchi ambazo zilikuwa za kibepari hazikuwa na maendeleo kuliko Tanzania nadhani ni kichaka cha kujificha tu, aidha kukwepa ukweli au kutoangalia mambo kwa mapana. Mifumo yote ya uzalishaji (Modes of Production) kuanzia utumwa, ukabaila, ubepari na ujamaa huwa na sifa zinazofanana, lakini leo hii ukisema uchukue mfumo wa ubepari na kuuanzisha kwenye kila nchi duniani kama mfumo rasmi wa uzalishaji nakuhakikishia lazima utapata matokeo tofauti.
Katika haya matokeo utakuta nchi ambazo zimefanikiwa sana na kutajirika, lakini kuna nchi ambazo zitakuwa zimefeli sana na kuwa masikini. Hili litatokea hata pale ambapo utatumia ujamaa kama ndiyo mfumo wa uzalishaji duniani kote. Sasa nini kinapelekea matokeo tofauti, tunakuja kwenye hoja yangu sasa: Kila nchi ina mazingira yake ambayo yanafanya iwe tofauti na nchi nyingine. Hivyo kupima maendeleo ya nchi moja kwa kuangalia mafanikio ya kiuchumi ya nchi nyingine, siyo jambo sahihi sana.
Nikupe mfano hai, hebu tuangalie The Structural Adjustment Programme (SAP), wengi wanadhani huu mchezo ulianza na nchi za Afrika. Lakini ulianza barani Ulaya kipindi cha The Marshall Plan, sema tu ulikuwa unafanywa na Marekani na siyo World Bank (WB) na IMF. Ulaya ilifanikiwa kiuchumi na kuna nchi zilitajirika sana tu, lakini nyingine zikafeli na kuishia kulaumu. SAP zikapelekwa Latin America ambapo nchi zilifanikiwa sana kiuchumi, lakini SAP zilezile hazikufanikiwa barani Afrika. Unadhani kwanini hazikufanikiwa ????
Mwaka 1998 Mwalimu Nyerere aliwakemea wazungu hadharani ndani ya mkutano akisema kila nchi ina mahitaji yake, hivyo kutumia sera ya jumla jumla kumesababisha matatizo. Akasema walimkosoa sana lakini wao wamefanya nini. SAP hazikufanikiwa Tanzania, lakini Argentina zilifanikiwa. Unadhani bado ni sawa tu kuendelea kulinganisha nchi ????
Pili, Sasa basi haya kabla ya kukimbilia huko kwenye GDP na kuanza kufananisha Tanzania na nchi nyingine, basi tuanze kwa kupima hali ya maisha ya watu kwenye nchi husika kwa kutumia nyenzo za kisayansi kama Human Development Index (HDI) ambayo hupima Life Expectancy, Per Capita Income Indicators na Education, vitu ambavyo ni msingi ndani ya taifa moja peke yake.
Haya sijayasema mimi MALCOM LUMUMBA, mchumi mkubwa duniani Prof Mahbubi Ul Huq ndiyo aliyekitengeneza hiki kipimo na kusema kitumike kupima maendeleo ya nchi husika kabla ya kutaka kufananisha taifa moja na jingine. Lengo la kufanya hivi ni kwasababu ukuaji wa ukuaji wa uchumi (Economic Growth) vinaweza visihusiane kabisa na raia wa kawaida kuwa na maisha mazuri ( Personal Well-being) au kupunguza utofauti wa vipato (Level of Inequality). Ntafurahi sana endapo Mkuu Kalamu1 utanirekebisha katika hili na kunipa kitu kipya kichwani,......
Hebu tuje sasa kwenye hoja yako ambayo wewe mwerevu uliyediriki kabisa kuniita mimi mpuuzi. Unauliza nchi gani ya Afrika ambayo haikuwa ya kijamaa lakini ilipata maendeleo kuliko Tanzania, ukataka kabisa na mifano. Mimi nijibu kama ifuatavyo: Mosi, kipimo sahihi cha kuangalia maendeleo ya nchi ni kuipima nchi husika kwa kuangalia maisha ambayo watu wake wanaishi kwanza, siyo kulinganisha GDP na nchi zingine. Hapa hatuwezi kulinganisha Tanzania na nchi nyingine kwasababu maendeleo hayo in Monetary Terms Alone, but also Non-Monetary Terms.......
Mwanauchumi nguli duniani wa kizazi chetu, ambaye ana tuzo ya Nobel ya Uchumi Prof Joseph Stiglitz anasema hivi, ukilinganisha Uchumi baina ya nchi peke yake hauwezi kufika kwenye jawabu sahihi. Hivyo yeye akapendekeza nyenzo kama The Capability Approach, ambayo hujikita katika kuangalia uwezo binafsi wa watu katika kufanikiwa kupata mafaniko binafsi endapo wataamua kufanya hivyo wakipewa uhuru.
Unaweza kusema watu wako huru kuzalisha au kutumia rasilimali zao na haki hizo ziko kikatiba, lakini kiuhalia hayo ni maneno matupu na watu wachache sana ndiyo huwa na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. Haya anayasema Prof Amartya Sen, siyo mimi. Sasa tujiulize swali la msingi kabisa tukitumia The Capability Approach: Hivi ni watanzania wangapi (Binafsi) wana uwezo wa kuzitumia rasilimali zilizopo Tanzania katika kujikwamua kiuchumi ??? (Tupime hili tukilinganisha kipindi cha Ujamaa na kipindi chetu hiki cha leo)
NB: Wajamaa waliwatengenezea watanzania uwezo binafsi wa kutumia rasilimali zao ????
Prof Joseph Stiglitz anasema hivi, tusipime uchumi kwa kuangalia "Gross" bali "Nets" ambapo ametaka tujikite kutazama hali ya wananchi wenyewe. Hivyo nikitazama watanzania, uwezo na rasilimali walizonazo hawakutakiwa kuwa hapa walipo leo hii. Hivyo kusema kwasababu nchi nyingine zilifeli basi Tanzania ni sawa kufeli ni hoja inayonishangaza sana. Lakini niko wazi kufundishwa zaidi, maana sifahamu kila kitu......
Mwisho kabisa, naongezea kitu kinaitwa Adjusted GDP's Approach. Hapa wachumi wanasema kwamba nchi husika kupimwa yenyewe ni jambo sahihi zaidi kwasababu maendeleo ya nchi hayatakiwi kuangaliwa katika nyanja ya uchumi peke yake (Monetary Terms Only). Hivyo lazima tuanze kuipima nchi husika kwenye muhimu kama utoaji wa afya bora, elimu bora, utunzaji wa mazingira n.k.
Hapa namaliza na maswali ya msingi kabisa: Watanzania wangapi walipata afya bora na elimu kipindi cha Ujamaa ??? Je, vipi kuhusu haki za msingi za kiraia (Basic Human Rights) pamoja na taasisi za kiraia ambazo zilitakiwa kutengenezwa ili kulinda haki za raia ??? (Kumbuka Karl Marx, anasema Human Rights are nothing rather than manifestations of The Capitalist Superstructure )
Mzee Nyerere naye akaamini kabisa akafutilia huko The Bill of Rights, wakisema It's a luxury we cannot afford.
Hivyo basi, mimi nasema tena: UJAMAA ulifeli na ukitaka kutumia ushauri na akili zilezile zilizotusababishia haya matatizo tuliyonayo leo basi endelea. Lakini pia ukiamini kabisa kwasababu mataifa mengine ambayo hayakuwa ya kijamaa yalifeli basi na sisi hatukuwa na namna, nakutakia kila la kheri mkuu.
Hapa barani Afrika kuna watu wanaamini kabisa kwamba ukoloni ndiyo umetuweka hapa tulipo, AND NOTHING IS EVER THEIR FAULT. Lakini wanasahau kwamba kuna nchi zilitawaliwa na wakoloni ila zikapiga hatua kubwa sana kiuchumi kuliko wengine.
Karibu tujadili....................