Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

MIJITU ya Bara bana!
Kweli unamsomesha mchumba?
Hujajifunza bado kwa yaliyo wapata WANDEWA walio somesha wachumba zao?
Sikuhurumii aisee
UKOME kilanga komo tunasema sisi watu wa Pwani
 
wewe ni kubwa jinga baba zima unazidiwa akili na katoto kama ako...siku nyingine ujifunze MWANAMKE WAKO SIO NDUGU YAKO
 
Tafuta album ya westlife au backstreet boys.. sikiliza.. kunywa..lala.. amka kesho asubuh jiangalie kwene kioo.. sema maneno haya.. " She was lucky to have me n not the other way around."
Sahau.. songa mbele..subiria uliepangiwa kuwa nae..
All the best.
 
Mkuu niamini umeandalia mke bora kuliko huyo.Nilikuw na galfriend na tulipanga tuoane akimaliza chuo.Nilikuw namgharamia hasa.Alipofika mwaka wa pili from no where akanambia hahitaji kuwa nami tena.Nilimuuliza sabab akanambia hataki tu kuwa na uhusiano na mwanaume yeyote.Niliumia san lakn nilipga moyo konde.Kwasasa nina mke mzur,ana masterz na kazi nzur baada ya kuw nae kweny uhusiano nae kwa miaka 8(nikimsubir amalize kusoma)
Amini,utapata mke bora!!
 
ndugu yangu wanawake wako complex sana na siyo rahisi kuelewa wanaridhika nini. Kama ulifanya yote kumshawishi hakukubali kuwa mume, Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inasema zawadi kwa mwanamke hazirejeshwi baada ya uchumba kuvunjika. Jitahidi tu huko Polisi labda utafanikiwa!
 
Natamani nikutukane.. Mchumba hasomeshwi.. Labda kama amekuzalia.. Pumbavu kabisa.. Tuwaimbie mara ngapi? Hadi boda boda na baashinya madala dala wameandik kuwa "mchumba hasomeshwi mjombaaaa"


labda tuanzishe jukwaa la WASOMESHAJI WACHUMBA ili wapeane visa vyao maana tumechoka sasa. (in voice of mzee pinda)
 
Pole Mkuu. Vumilia tu na kama ikikupendeza futa tu kesi na uendelee na maisha yako ya kawaida kama zamani wakati ukiwa hujamuona binti huyo.
Anyway, inauma lakini utafanyaje wakati ndege kashakukimbia?
 
Imeniuma sana japo sio mm yaliyonipata ni HV tujifunze kupitia haya kumsomesha mchumba/mke ni kujizika fikra majukumu wawe wanafanya baba/mama/ndugu over!!!!asilimia kubwa sana huwa wanajutia mchakato huo!!!blessed

Masinki
 
YANI SIJUI UNAWAZA NINI NA HIYO KESI NAONA KAMA UNAJICHIMBIA KABURI TU...ACHANA NA KILA KITU FANYA YAKO...AF MBONA KILA SIKU TUNASEMA MCHUMBA HASOMESHWI...HAAA ANYWAY HUKUJUA....ULISIKILIZA MANENO YAKILAIISHI YA MAMA MZAZI ETI KAMA UNA NIA FANYA HIKI....HUWA SIAMINI HAYO MANENO....ETI KU PROVE KITU UWAFANYIE KITU...MFANO SAMSON DELILA ETI KAMAUNANIPENDA NIAMBIE NGUVU ZAKO ZATOKA WAPI..COMDITION KAMA HIZO KWANGU NI VOID...MARA OO KAMAUNANIPENDA NINUNULIE VOCHA NA ZINGINE NYINGI...HUKO NI KUTEGWA TU NA KUPELEKESHWA,...KAMA UNANIPENDA NIONE MWEZI UJAO...LA SIVO NAOLEWA KWINGINE....SO NUL VOID.....MWISHO POLE SANA
 
Hmmm, inauma! lkn hakuwa wako Huyo! Hold ur peace, let her go!..... Lkn usije ukamuadhibu mwanamke mwingine, lwa makosa ya mwanamke mwingine!
 
Yapo Sana hayo.... acheni kuwavizia wanafunzi wakati wanasoma... Mwanamke ukiwa naye mbali ndani ya miezi mitatu ni kosa kubwa sana wewe ndio wa kulaumiwa... hivyo Tulia
 
Piga moyo konde mkuu, then move on..mwanaume wa kweli huwa halii kihivyo.
 
"Ghost In Real Life(girl)" duuuuh kumbe wanawake ndo wanaroho mbaya hivyo, mkuu ahsante kwa fundisho lako
 
That is not your wife brother,ni mke wa mtu mwingine.Pole sana.Badala ya kuanza kuhangaika mahakamani kwanini usiachilie then maisha yakaendelea?

Futa mawasiliano na yeye ,ndugu zake na yoyote anayemuhusu.Utarikava tu na itakuwa ni experience kwenye maisha yako.

Kumbuka whats goes round comes round.
 
Huyu jamaa alete mrejesho ilikuwaje
 
mshukuru Mungu kwa kila jambo. pengine Mungu kakuepushia msalaba wa milele. tulia jipange upya
 
Be above them,huyu hakukupenda ,jamaa aliemuoa ni a brother hastahili kero zako ,achana na hilo samehe na watakie kila la kheri,narudia MCHUMBA HASOMESHWI HATA KWA UTANI
 
Ulikuwa kichwa maji hawa watu hawana huruma ilikubidi umtundike mimba Kwanza ndio aende shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…