Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Kubali kilichotokea kwanza,pili let it go.. Km wajisikia kulia lia tuu itasaidia kuondoa uchungu na mzigo unaousikia moyoni.. Life is too short don't let anyone still ua happiness. Watu wanakutana na changamoto nyingi ktk maisha ila wanajipa moyo na kusonga mbele. Waweza pia songa mbele... Yupo wa ubavu wako
 
u deserve it na kwa miakali ya kijinga huenda ndugu wako wa damu alihitaji msaada wakohukumsaidia kisa binti
 
kimbelembele chako hicho. kwa hayo majukumu mwenzio alikuchukulia kama mzazi atembeae na binti yake sasa kapata mume.
 
Pole yako - Maishani mwangu sitokuja kumsomesha mwanamke wangu a.k.a mpenzi wangu kamwe.! Mara nyingi ukiwasomesha baadae hukugeuka na wanaenda kuolewa eidha na watumishi wenzao au vibopa au wasomi wenzao.du nakusikitikia bure.
 
Dear brothers and sisters, uchumba sio ndoa. Usimfanyie vitu vya gharama mchumba. Anaweza kuja kuwa mume/mke wa mtu baadae huyo. Ni mke wako ama mme wako ndio unatakiwa kumgharamia kwa akili yako yote na mali zako zote Na nguvu zako zote.
 
Hey... Pole mkuu. Hayo ndio maisha, na hayo ndio mapenzi. Najua kuwa amekuumiza lakini haikuwepo uradhimu wa kumpeleka mahakamani. Hiyo kesi ifute, sahau, Cheka na endelea na maisha. Ni vitu vya kawaida hivyo hata visikuumize kichwa. Binadamu wote duniani hapa tunapita. Siku ukija kujua dhumuni la sie kuumbwa na kuishi hapa duniani, basi utaanza kuwaelewa binadamu wote mazuri na mapungufu yao. Samehe, Cheka na jaribu kusambaza upendo kwa kadri uwezavyo. Ndio ushauri wangu huo
 
Mimi niliwahi kuumia sana, du kweli mapenzi ysnaumiza!!! Pole ndugu I do remember ila siku hizi nimewadharau sipendi nawapiga mno siku hizi alafu wanaongezeka tu .
Nakushauri upotezeeee tu, kaaa mwaka m1 single accumulate your wealth then utapata mwingine.
 
Pole sana mkaka kwakuingia chaka, ushauri wangu samehe mwachie Mungu malipo hapa hapa duniani iko siku utaleta mlejesho, omba uzima tu fanya maombi utampata akupendaye lakini usifanye haraka kutafuta tulia kwanza pressure ipungue la sivyo utaangukia chaka lingine, nakushauri kama mwanamke ninaye jitambua, hata wanawake huachwa sana anakataa wachumba wengi kisa mchumba anasoma siku isio kuwa na jina mchumba anakuja na mke, piga moyo konde wewe si wakwanza kisasi cha Mungu je! Kama Mungu kuepusha na janga kubwa zaidi ya hilo achana naye piga maombi.
 
Pole aiseee.

Haya mambo ya kuchukia yapo kote kote.

Kuna mtu anakufanyia vituko hadi unawaza huyu shetani au binadamu, lakini unakumbuka mwanzo hakuwa tu binadamu ila malaika mwema kabisa.

Me nawachukia wanaume hakuna mfano ila mwisho wa siku wapo wenye tabia nzuri na wasiobadilika kabisa kutoka malaika binadamu hadi shetani. Hawa wakibadilika saaaaaanaaaaaa wanaishia kwenye ubinadamu
 


Wewe ni Mwanamke au Mwanaume? Na ni born town au umetoka Tarime?
 
Nawashangaa sana watu wanajitwika mizigo ya kuwasomesha wanawake wasiokuwa na nasaba nao.....!
Labda tu Unaweza msomesha mkeo wa ndoa lakini eti mtu anaingia gharama kusomesha girlfriend, mchumba au sijui hawara au nyumba ndogo hapo baadae yakija kutokea ya kutokea utamlaumu nani kama si kujilaumu mwenyewe tu...!
Somesha mwanao wa kike au dadako kwani hao hata wakijaolewa ni watu ambao wanakuhusu na hata ikitokea bahati mbaya wameachika au kufiwa na wenzi wao basi hawataweza kunyanyasika au kukusumbua sana kwani watakuwa na elimu ambayo itawasaidia kuwa na kipato...
 
Bahati mbaya Nimechelewa kujua
Relax...jipe muda na amini utasahau tu. Kupelekana mahakamani sizan kama no sulihisho zaidi zaidi unaweza ongeza machungu na ukapoteza tu muda wakom. Ts truly hurt but just believe its never meant for you. Am very sory for you!
 
Wanawake bhana hawana maana sometime ...ingekuwa wao uone wanavyopiga majungu ...Anyway MWALIMU WA WAONGO,WAHUNI,WANAWAKE NA WANAUME NI MMOJA DUNIA NZIMA....Kaka huyo hiyo ndoa yao haina miaka sita maadamu kakusaliti mungu atakulipa, vumilia piga kazi zako forget and move on..
 
Hesabu hiyo kama hasara ktk investment. Kama amekukukera sana na kukuondoa kwenye fomu, kuendeleza kesi kutakupotezea muda, fedha, akili na maendeleo. Hesabu hiyo ni hasara, Muombe Mungu na start another episode. Pole sana lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…