Nimemuacha lakini naumia mimi

Sasa kiongozi unaposema hujawahi kumkuta na mvulana una maana gani? Kumkuta kitandani? Mbona unadai alienda kabisa Arusha kwa Jamaa?

Anzia upya tu ndugu yangu sehemu ingine, huyo haki nakuapia hakufai. Najua unaumia sababu ulimpenda/unampenda sana ila kama yeye hakupendi sasa kuna faida gani? Utakonda, utashindwa kufanya kazi mwenzako hana hata muda na wewe, kama usemavyo ni kweli kuwa ulishaongea nae hadi kwa kutumia ndugu zake na haikufaa basi 'simama, kung'uta makalio' anza mwendo sehemu ingine............
 
Pole sana ndugu yangu, naguswa na maumivu yako. Mi uwa naamini kuwa kila tatizo lina maana na mwisho wake pia. Kama unahisi hayo mapungufu yake yanarekebishika basi mrudie, lakin hayarekebishiki basi usimrudie. Piga moyo konde songa mbele hayo maumivu yataisha tu kadri siku zinavyokwenda na ipo siku utampata msichana mtayependana naye kwa dhati. Ila usiharakishe kuingia kwenye uhusiano mpya kuepuka kuingia mkenge kwa asiyefaa zaid. Maumivu ya kumwacha mpenzi asiyejua thamani ya kupendwa yanauma sana. POLE SANA.
 
Endelea kushika mapembe kama bado unahitaji! It is very obvious kwamba hupendwi ulikuwa unajipendekeza tu kwa huyo dada! Mwanamke anayekupenda na kukuthamini hawezi hata dk1 kukuumiza roho yako!
 
Kama alikutesa sana huu ni wakati wako wa kukaa mwenyewe na kutafakari jinsi yakuendelea na maisha yako
huwezi kujua Mungu kakuepusha na nini, wako yuko katulia ambae mtamatch kwa kila kitu ni muda tu
 
wana JF,

nashukuruni sana kwa ushauri wenu, nimepata faraja sana na mungu awazidishieni hekima na busara,

kweli nashukuru pia kuwa katika forum ambayo napata msaada wa kimawazo

mungu awabariki sana,

ahsanteni.

dah kaka kila nikiangalia avatater mkono unagoma kuendelea
 
Gangwe
Naona wewe ndio watu wanasema umezama katika lindi la mapenzi.
Lakini kama alisema hivyo, ujue alifanya na ndio maana akasema anakudanganya, katika mapenzi kujaliana ni muhimu, sasa mpenzi gani huyo tena ambaye hata hakujali, kila siku unateseka wewe tu.. nakushauri kimbia.. mbona mabinti wengi tuu, Gangwe kama wewe lazima utapata mrembo mwingine bana, komaa kigangwe na usirudi nyuma, atakutoa roho huyo!

aah kumbe wewe ni Gango nilidhani Gangwe!
 
Aisee umeongea kwa uchungu hadi nahisi umemwaga chozi. Pole kaka. Kupenda halafu hupendwi inaumiza sana. Hujafanya kosa kumuacha, tunapokuwa na wapenzi tunatarajia furaha. Kama upo na mtu na bado unakosa furaha hakuna sbb ya kuendelea kumng'ang'ania.
Lazima kwa sasa utaumia kwasababu kuna mambo mengi unayamiss ila kadri siku zinavyoenda utaona kawaida.
Jaribu kutomfikiria kama kweli umeamua kumuacha. Kama unahisi huwezi kuacha kumfikiria basi fikiria mabaya yake zaidi kuliko mazuri.
Kama unahisi furaha yako ni yeye tu wa kuikamilisha rudisha majeshi.
 
Kwa nini uumie huku mwenyewe muhusika yupo? mrudia ili muweke mambo yenu sawa, mwambie nini hupendi ili asirudie hiyo mistake tena
 
<br />
<br />
Pole kaka!
Usisahau tena hii maana Girlfriend si mke! Boyfriend si mume!.
Ina maana mlikua kwenye majaribio kama wengi wanavyomaanisha.
Tumia nguvu nyingi kutafuta na kupanga maisha ili ukimpata mwenye huruma juu yako uishi nae maisha mema .
Kumpata mume/mke ni kama kutafuta kazi inayolipa kwa kiwango kizuri. So! Endelea kuwa mpole na kujipanga upya!.
 
Kimbia fasta,huyo hakuwa anakupenda na inaonyesha alikuwa anakutafutia kila sababu umpige chini sema ulikuwa hujashtuka ukaendelea kuwa kinganganizi.uko sahihi kufanya maamuz kama hayo.maumivu hayo ni ya kawaida kumwacha au kuachwa na umpendaye,songa mbele.
 
Kosa ulilolifanya ni kumruhusu akueleze yote yale, ile amesema tu anaenda kukaa kwa mvulana aliyemtafutia kazi ungemwambia aishie hapo hapo na safari yake ungeifuta rasmi na kama angeng'ang'ania hapo ulikuwa na haki ya kujitenga naye.
 
Mkuu ..hiyo picha ya avatar ni yako..inaonekana ni mtu wa mangumi..na manundu ..maana hata mimi nimeogopa kuandika..Anyway...labda naye ameshindwa vumilia hayo(Joke)...

Tafuta mwingine wako wengi..
 
Mkuu umeandika kwa hisia mpaka imenigusa sana...sikushauri umrudie kaka maana halitakuwa suluhisho la yeye kuacha kukutesa na kukusaliti...jua kwamba kuna gharama za kuachana na kamwe maumivu upatayo sasa yasikufanye urudi nyuma.
Piga moyo konde uendelee mbele na maisha yako...utampata atakaekupenda sana kama utakavyompenda wewe.
This too shall pass.
 
nashukuruni sana wana JF kwa mawazo yenu yenye busara! ama kwa hakika hii ndio faida mojawapo ya kuwa nanyi

ahsanten sana!
 
nashukuruni sana wana JF kwa mawazo yenu yenye busara! ama kwa hakika hii ndio faida mojawapo ya kuwa nanyi

ahsanten sana!


Avatar yako inatisha bana!!
 
mapenzi mengine bhana,
we umemwaga mtu bado tena unaumia,!!!!!
Mrudie basi,
au unaumia baada ya kuona wenzio wanafaidi?
NWY, Nikupe pole kwa kupenda bila mipaka, kuamini kilicho ndani ya moyo wa mwenzio na kuamua kujiengua lakini bado unalialia....
 

Pole sana Mkuu, unaposema alikuambia kua anakudanganya unamaanisha nini? Kwamba alikua haishi na huyo jamaa au? je kwa uchunguzi wako umebaini nini juu ya mahusiano ya huyo jamaa?

Ushauri Wangu:
1.Kama unaumia ni dhahiri kwamba bado unampenda, na kidonda cha kuachwa/kuachana na mtu aliyeujaza moyo ni kikubwa sana, yawezekana kovu likadumu siku zote za maisha yako. Namaanisha hata mkiachana kabisa, ukawa na mtu mwingine naye akawa na mwingine, yawezekana usim-feel utakayekua nae maana yuko bado mawazoni mwako. Na utakua unaumia vikali kila ukimuona na huyo mpya atakaye kua nae.
2. Nabaini kuna tatizo flan katikati yenu, yawezekana hamjawekana wazi ni vitu gani mnapenda kufanyiwa/kufanyiana katika mapenzi. Mara nyingi wanaume ni wadhaifu sana kwenye mambo madogo ambayo wanawake wanayachulia serious sana. Namaanisha unaweza kua unamuudhi kwa vitu vingi bila wewe kujua na anaamua kufanya revenge kwa namna hiyo. Hilo linatokea mara nyingi kama hamna uwazi na uhuru wa kutosha katika mahusiano.
3. Mtafute, kaa nae, muweke huru ili akuambie kilichopo moyoni mwake na muyaongee yaishe. Naamini mahusiano yenu yanaweza kua mazuri na mapya tena na kama mtaheshimu mawazo na hisia za kila mmoja wenu mtakua na maisha yenye furaha forever.

Ndio mawazo yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…