Nimemuacha lakini naumia mimi

Kuwa wewe bila yeye. Huyo hakukupenda hata chembe, na amekuwa akitafuta chance ili umuache ulikomaa.

Ushauri, ishi wewe kama wewe, siyo wewe kama yeye.
 

Bwana mdogo Gonga Mbili;
Naona kama unatafuta justifications/excuses za kurudiana naye. Nimeshawahi kuona wasichana wa tabia ya namna hiyo uliyoitaja, japo si katika mahusiano kati yao na mimi. Wamekuwa wakihusiana na watu wengine halafu bahati mbaya au nzuri mahusiano yao yanatokea kuwa exposed kwangu either kama rafiki au ndugu wa karibu. Sikushauri umrudie au usimrudie ila jua kuwa ukimrudia uwe tayari kwa mojawapo tu ya mambo mawili yafuatayo:

1. Uhusiano ulioimarika sana na kubadilika kwa mpenzi wako kiasi kwamba utampenda kuzidi hata ilivyokuwa awali;

2. Uhusiano wa ajabu utakuja kutokea aidha immediately au baada ya mda kidogo. Anaweza kukutegea hadi akawa na uhakika kuwa umeamini kabadilika halafu umerudisha tena moyo wako kwake kuliko hata mwanzo, halafu ndiyo anakuja kukulipua vizuri, analeta za masika ukilinganisha na za sasa.

Wasichana dizaini hii huwa ni malimbukeni halafu wana akili kama imefyatuka kidogo, na mara nyingi wanakuwa ni waropokaji.

Anyway, just in case utashindwa, unaweza ukanitaarifu nirudiane naye mimi!
 
Wenzetu wazungu wanamsemo wanasema 'Pain is love'. Najua hali uliyonayo na unavyojiskia, kwasababu na mimi yalishanikutaga hayo zamani, ila usije ukafanya kosa ukamrudia huyo mwanamke, achana naye. Usiwe muoga kuanza upya, na anza upya sasa, yaliyopita si ndwele, utampata ambaye atakupenda na kukuthamini na atakayekuwa my wife wako.
 
Pole sana ndugu hayo ni mapito 2 binafsi nilipitia kipindi kama cha kwako niliacha kama wewe ilinipa wakati mgumu sana kwa kile kipindi lakini namshukuru Mungu nimesahau yote na maisha yanaenda kikubwa mwombe Mungu akusaidie uvuke salama kwasababu hapo ndipo wengi wanapoaribikiwa
 
mh huo mzaha sasa hakuna mapenzi ya kweli hapo huyo msichana anakuchezea, maana minavyojua msichana akiwa yuko siriazi na mtu hawezi kuwa na mzaha kiasi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…