Nimemuota marehemu

Nimemuota marehemu

SamuraiJack

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2017
Posts
225
Reaction score
239
Habari wanajukwaa?

Bila kupoteza muda ngoja nirnde moja kwa moja kwenye hoja. Nimekuwa nikimuota marehemu baba yangu mkubwa mara kwa mara japo alipata kufariki 2013 (Mungu amlaze mahala pema).

Japo alinilea toka udogoni kama mzazi wangu vile na kunichukulia kama mtoto wake. Nimekuwa nikimuota mara kwa mara tukiishi maisha yetu ya zamani kama muendelezo hivi. Na leo usiku pia nimemuota.

Hii katika ulimwengu wa kiroho inamaanisha nini?

Rakims Mshana Jr
 
Kuna mtu alisema ukiota ukiwa na mtu aliye fariki maana yake roho ya mauti kimwili au kiroho inakunyemelea.

Siku akija akisema twende zetu niliko ukikubari ndo habari yako itakua imeishia hapo.
 
Ni kawaida km Ulikuwa na Utaratibu wa kumuombea Dua kila baada ya muda fulani,Ule muda ukipitiliza Huwa anakumbushiaa!!! Kumbuka Dua ndio Chakula cha Marehemu.
Kwanini marehemu anaombewa?
 
Ni kawaida km Ulikuwa na Utaratibu wa kumuombea Dua kila baada ya muda fulani,Ule muda ukipitiliza Huwa anakumbushiaa!!! Kumbuka Dua ndio Chakula cha Marehemu.a

Mkuu, hakuna kama hiko mkuu, marehemu keshaenda na kamaliza mwendo wake. Huko alipo hana kumbukumbu tena. Haya ya kuwaombea dua sijui misa n.k ni mapokeo ya kibinadamu. Matendo yake yatafutana naye, Roho yake imemrudia muumba wake aliyempa na mwili wa udongo upo Kaburini akisubiri siku ile ya kusimama mbele ya Mungu kwa ajili ya hukumu.

Umarehemu wetu na kupumzika au kutopumzika baada ya mauti unaandaliwa tukiwa hai na si dua,misa,sala na maombezi toka kwa walio hai.
 
Habari wanajukwaa?

Bila kupoteza muda ngoja nirnde moja kwa moja kwenye hoja. Nimekuwa nikimuota marehemu baba yangu mkubwa mara kwa mara japo alipata kufariki 2013 (Mungu amlaze mahala pema).

Japo alinilea toka udogoni kama mzazi wangu vile na kunichukulia kama mtoto wake. Nimekuwa nikimuota mara kwa mara tukiishi maisha yetu ya zamani kama muendelezo hivi. Na leo usiku pia nimemuota.

Hii katika ulimwengu wa kiroho inamaanisha nini?

Rakims Mshana Jr
Unamuota katika mazingira gani?
 
Kuna mtu alisema ukiota ukiwa na mtu aliye fariki maana yake roho ya mauti kimwili au kiroho inakunyemelea.

Siku akija akisema twende zetu niliko ukikubari ndo habari yako itakua imeishia hapo.
story za vijiweni hizi acha kupotosha watu ww
 
Habari wanajukwaa?

Bila kupoteza muda ngoja nirnde moja kwa moja kwenye hoja. Nimekuwa nikimuota marehemu baba yangu mkubwa mara kwa mara japo alipata kufariki 2013 (Mungu amlaze mahala pema).

Japo alinilea toka udogoni kama mzazi wangu vile na kunichukulia kama mtoto wake. Nimekuwa nikimuota mara kwa mara tukiishi maisha yetu ya zamani kama muendelezo hivi. Na leo usiku pia nimemuota.

Hii katika ulimwengu wa kiroho inamaanisha nini?

Rakims Mshana Jr
kma we ni Muislamu muombee sana dua mzazi.wako huyo na waambie wanawe wamuombee sana dua baba yao mna hicho ndo kitu anachokihitaji kwa sasa
ukimaliza kuswali ktka zile sala tano Muombee dua au kma unaweza kuamka usiku pia muombee sanaaa
 
Back
Top Bottom