Nimemuota marehemu

SamuraiJack

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2017
Posts
225
Reaction score
239
Habari wanajukwaa?

Bila kupoteza muda ngoja nirnde moja kwa moja kwenye hoja. Nimekuwa nikimuota marehemu baba yangu mkubwa mara kwa mara japo alipata kufariki 2013 (Mungu amlaze mahala pema).

Japo alinilea toka udogoni kama mzazi wangu vile na kunichukulia kama mtoto wake. Nimekuwa nikimuota mara kwa mara tukiishi maisha yetu ya zamani kama muendelezo hivi. Na leo usiku pia nimemuota.

Hii katika ulimwengu wa kiroho inamaanisha nini?

Rakims Mshana Jr
 
Kuna mtu alisema ukiota ukiwa na mtu aliye fariki maana yake roho ya mauti kimwili au kiroho inakunyemelea.

Siku akija akisema twende zetu niliko ukikubari ndo habari yako itakua imeishia hapo.
 
Ni kawaida km Ulikuwa na Utaratibu wa kumuombea Dua kila baada ya muda fulani,Ule muda ukipitiliza Huwa anakumbushiaa!!! Kumbuka Dua ndio Chakula cha Marehemu.
Kwanini marehemu anaombewa?
 
Ni kawaida km Ulikuwa na Utaratibu wa kumuombea Dua kila baada ya muda fulani,Ule muda ukipitiliza Huwa anakumbushiaa!!! Kumbuka Dua ndio Chakula cha Marehemu.a


Umarehemu wetu na kupumzika au kutopumzika baada ya mauti unaandaliwa tukiwa hai na si dua,misa,sala na maombezi toka kwa walio hai.
 
Unamuota katika mazingira gani?
 
Kuna mtu alisema ukiota ukiwa na mtu aliye fariki maana yake roho ya mauti kimwili au kiroho inakunyemelea.

Siku akija akisema twende zetu niliko ukikubari ndo habari yako itakua imeishia hapo.
story za vijiweni hizi acha kupotosha watu ww
 
kma we ni Muislamu muombee sana dua mzazi.wako huyo na waambie wanawe wamuombee sana dua baba yao mna hicho ndo kitu anachokihitaji kwa sasa
ukimaliza kuswali ktka zile sala tano Muombee dua au kma unaweza kuamka usiku pia muombee sanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…