Nimemzaba makofi baada ya kugundua anataka kuniibia akidhani nimelewa

Nimemzaba makofi baada ya kugundua anataka kuniibia akidhani nimelewa

DR SANTOS

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
12,846
Reaction score
28,106
Sijui kama nilitumia busara Kwa hii ishu au laa ila Wahudumu wa bar mostly ni wezi na kamwe usithubutu kumpeleka kwako hasa ukiwa umelewa, yaani Kwa kifupi Bora umchukue yeye akiwa amelewa kuliko muende wote mmelewa utaja ibiwa my friend.

IPO hivi, Jana katika harakati za kumwagilia moyo meza yetu ilikua imechafuka mbaya kali zilikuepo laini pia yaani ni spirit na beer, nyagi na energy huku pembeni nikishuhidia liverpool akiliwA Chuma tatu na Brighton😂

Taratibu wachumba wakaanza kujileta na tukaanza ku share drinks kwenye meza yetu. Kuna mmoja yeye alikua tu kwenye meza ila hanywi chochote nilipomdadisi akadai yeye alilewa sana mchana Kwa mda ule hakuhitaji kunywa Kwa wakati ule ila beer ilipoisha alikua wa kwanza kubeba chupa na kuzihifadhi vizur.

Sasa nikawa nachati chati na mama la mama huku simu zangu nimeweka mezani, kumbe yule dada ananilia target tu anipige simu.

Bahati mbaya pombe ikanimwagikia kwenye suruali, kitendo Cha kuinuka nijifute nakuta simu hazipo😬😬😬
Afu light ilikua low Kwa haraka haraka nikapepesa macho namuona yuleee ndo anatoka nje aise niliwahi kimya kimya nikamfuata nikamvutia ili asinijazie nzi pale pembeni, nikamwambia rudisha simu zangu😬 mimi sijalewa nimekuona ukibeba akasema we kaka viipi?

Nikamtahadharisha kwamba sirudii mara mbili statement bado aka resist Nikamzabua Kofi la shavu akaanza kulia na kuomba msamaha na kurudisha simu zangu mbili Google pixel na docomo Aquos.

Mwisho akaomba msamaha akadai ana matatizo simu yake imekufa maisha ni magumu sana mwanae anaumwa nyumbani wanamtegemea😓😓

Nilimuonea huruma sana pamoja na yote nikampa elf 20 ila nilimsihi aache wizi baada ya hapo nikaamua kurudi tu nyumbani maana mood ilikata baada ya tukio lile.

Chini Kuna ka video
 
Usitupigie wahudumu wetu wakati mwingine chief tunawapata kwa taaabu sana


e4ce0220d1f94f80916d3c6085698e2e.jpg
Enjoy hii kitu kwako kwa Case 52,500
 
Mkuu kama ulimpa na hela kabisa baada ya huruma ya kiume kukupanda, ulishindwaje kwenda kumlala?
 
Back
Top Bottom