Nimenunua kilo ya mbegu za maboga 12000 Moshi

Nimenunua kilo ya mbegu za maboga 12000 Moshi

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Wadau,

Nikiwa nahangaika kupata materials ya lishe kwa ajili ya shangazi yangu mwenye kisukari.

Nilizunguka soko la mbuyuni Moshi kila kona kutafuta mbegu za maboga sehemu moja nilienda bei Kg 1 ni kuanzia 15000, nikajua hataki kuniuzia kwa sababu mwaka jana nilinunua 8000 kwa kilo.

Nikaenda kwa mwingine bei ndio hiyo, baada kuchoka nikaambulia aliyeniuzia 12000 kwa kilo moja.

Hoja yangu, watu wameamka na wamejua umuhimu wa hizi mbegu kwenye afya zao, haswaa kwa wanaume. Watafiti wetu muingie maabara mje na breed ya boga yenye uwezo wa kutoa mbegu nyingi, kwa sababu mbegu zake zimekuwa dili kuliko boga lenyewe.
 
huku Dar ni Elfu 8 tuu
.. mwaka jana ilikuwa 2500 tuu
 
Ni aina gani mkuu? Local breed au ya kisasa? Nipe mchongo niyalime nina bonde zuri sana
 
Khee huko moshi mmejaa matajiri huku kwingine bei hiyo unaweza pata hata kilo tatu au nne
 
Hizo Mbegu zako Mkuu zina rangi gani?kuna kama za kjani kidogo na za kama khaki kiaina.
 
Achana na hizo mbegu hata hiyo minofu yake hiyo n chakula kizur Sana kwa mifugo
 
Mi pia nnazo nipo Mbeya
Mfano pepita.JPG
 
Mkuu mbegu ya maboga ni dili Sana Kuna Yule mzungu maiko barabara ya machame analima na kuuza ulaya hizo mbegu
 
Daah nakumbuka enzi hizoooo huko kwetu kijijini tulukuwa tunatupa hizi
 
Back
Top Bottom