Nimenunua koti la mtumba lina pesa za Saud Arabia anaezijua anisaidie

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,750
Reaction score
2,283
Habari wana Jukwaa,

Kama kichwa cha habari hapo juu,

Siku chache zilizo pita Dar kulikuwa na mvua za hapa na pale, kwenye pita pita zangu nikakutana na muuza makoti ya mtumba, nikalipenda moja nikalinunua.

Baada ya kufika nyumbani nikawa nalisachi mifukoni ili nilifue, kwenye kimfuko kidogo cha ndani nilikuta kuna noti 5 za Saud Arabia.

Zimeandikwa hivi;
SAUDI ARABIA MONETARY AGENCY. ( ONE RIYAL 1)
ziko noti tano nimewaonesha na kuwauliza marafiki zangu wote hawazijui na mi nimeogopa kwenda sehemu za kubadilishia hela nikiwa na hela ambazo sizijui zina thamani gani, na Je zinatumika? Maana pembeni zimeandikwa 2012. Unaweza kupigwa pingu mwizi kumbe sijawahi dokoa hata mboga masikini wa Mungu.

Nimeleta kwenu humu kwa wanaozijua aniambie.

 
1 Saudi Riyal equals
606.39 Tanzanian Shilling
 
Riyal moja ni kama sh 600 , mara 5 kama 3000
 
Hizo thamani yake haizidi buku mkuu..
So hujatusua wala nini ww endelea kulegeza vyuma vilivyobanwa na J mnywa pombe..
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Duuuh kweli noma nilijua nimetoboa sasa
 
Ha ha ha Magu legeza kidogo, maana mara mtu kaokota fuko la hela...mwingine kaokota chuma anadhani madini[emoji23][emoji23][emoji23] hela haziji kirahisi hivyo jamani
 
Ha ha ha Magu legeza kidogo, maana mara mtu kaokota fuko la hela...mwingine kaokota chuma anadhani madini[emoji23][emoji23][emoji23] hela haziji kirahisi hivyo jamani
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]...
Yule jamaa alinimaliza kinomaa,eti kaokota fuko lina m250!!.
Muda huu nadhani atakuwa kalazwa hosp baada ya kuamka na kujikuta hana hata buku la vocha!!!.
 
Mleta thread pengine hajaenda job akidhani amesha yatusua maisha,

Hapa amesha pigia hesabu anaenda kungoa ile nyumba ya Lungumi inayo pigwa mnada
 
tumia kutongozea watoto wa kitanga au wazaramo.Ina thamani ikiwa hivyo kuliko ukibadirisha mkuu utashia kununua bia moja ya kirikuu
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]...
Yule jamaa alinimaliza kinomaa,eti kaokota fuko lina m250!!.
Muda huu nadhani atakuwa kalazwa hosp baada ya kuamka na kujikuta hana hata buku la vocha!!!.
Aliniacha hoi alivyosema wamehesabu watu wawili mpk asbh
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…