Nimenunua kuku wanne wa miezi mitatu

Nimenunua kuku wanne wa miezi mitatu

IJIGHA NDIO HOME

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2019
Posts
760
Reaction score
823
Habari wakuu, nanshukuru mungu nimenunua kuku wanne wa miezi mitatu shiling 5000 kila moja nategemea kila mwezi kuongeza wengine kumi.malengo yangu nataka niwe nakuku 20 wa mayai. Nimetengeza Banda kwa kutumia mabanzi.

Huku ludewa (NJOMBE) mabanzi Ni kutosha unajiokotea tu, nikanunua turubai kubwa kwa ajili ya mvua. Naombeni ushauri wenu kwa hapa nilipofikia.

IMG_20220128_072627_4.jpg
 
Inaonekana kuna baridi sana huko alafu hiyo W3 haipigi picha nzuri. Umesema kuku wa 3 ila mm nawaona 4 au hayo mengine madumu? Tecno W3 kitambo sana kabla ya simu zile zimu za waasi Tecno M23
 
Komaa nao wqkiongezeka leta mrejesho ila wakifa kwa mdondo pia usisite kuleta mrejesho
Kilala heri ndugu
 
Hongera mkuu, uthubutu ndio unaoleta tofauti, safari ya maili moja inaanza na hatua moja

Usikate tamaa kwa maudhi madogo madogo utakayopitia, siku njema zipo mbele.

Ukinunua batch ya pili wachanje mdondo utanishukuru kipupwe
 
Inaonekana kuna baridi sana huko alafu hiyo W3 haipigi picha nzuri. Umesema kuku wa 3 ila mm nawaona 4 au hayo mengine madumu? Tecno W3 kitambo sana kabla ya simu zile zimu za waasi Tecno M23
Tecno W3 niliitumia Mara ya mwisho ilikua mwaka 2015 mwishoni. Ko katika kubashiri kwako nikuambie tu mkeka wako umechanika. Pia inaonyesha Ni mvivu wa kusoma waachie waliouelewa uzi mku
 
Hongera mkuu, uthubutu ndio unaoleta tofauti, safari ya maili moja inaanza na hatua moja ...
Usikate tamaa kwa maudhi madogo madogo utakayopitia, siku njema zipo mbele.

Ukinunua batch ya pili wachanje mdondo utanishukuru kipupwe
Shukrani mkuu kwa ushauri wako
 
Habari wakuu, nanshukuru mungu nimenunua kuku wanne wa miezi mitatu shiling 5000 kila moja nategemea kila mwezi kuongeza wengine kumi.malengo yangu nataka niwe nakuku 20 wa mayai. Nimetengeza Banda kwa kutumia mabanzi. Huku ludewa (NJOMBE) mabanzi Ni kutosha unajiokotea tu, nikanunua turubai kubwa kwa ajili ya mvua. Naombeni ushauri wenu kwa hapa nilipo fikiaView attachment 2100704
Huyo mweusi mchinje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nikupongeze. Jipange sawasawa ufikie malengo. Zingatia chanjo na chakula. Iko siku utakuwa mbele za watu.
 
Inaonekana kuna baridi sana huko alafu hiyo W3 haipigi picha nzuri. Umesema kuku wa 3 ila mm nawaona 4 au hayo mengine madumu? Tecno W3 kitambo sana kabla ya simu zile zimu za waasi Tecno M23
Inaonekana hujui kusoma wewe.
 
Salut Mkuu,Kuku wanaonekana wana afya.
 
Mabanzi ni ya kujiokotoea?

Nipe Connection mkuu nahitaji mabanzi, kwa ajili ya banda la kuku kama wewe.

Kongole kwako kwa udhubutu, ukiwa na mbili ni rahisi kupata nyongeza ya moja.
 
Mabanzi ni ya kujiokotoea?
Nipe Connection mkuu nahitaji mabanzi, kwa ajili ya banda la kuku kama wewe.

Kongole kwako kwa udhubutu, ukiwa na mbili ni rahisi kupata nyongeza ya moja.
Kwa njombe Ni ya kujiokotea tu mkuu
 
Tembelea maduka ya madawa upate elimu zaidi pindi wakikabiliwa na magonjwa
 
Najuwa umewanunua ili wakuekue uwanyanduee [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom