Hili ni tatizo moja kubwa sana ambalo linaweza kupelekea kuanguka kwa nyumba (esp Ghorofa). Tatizo lenyewe ni kutozingatiwa kwa viwango kwenye hivi viwanda vya Nondo. Nondo kabla haijaingia sokoni inatakiwa ihakikiwe ubora wake ambapo hupimwa (Tensile strength - uwezo wa kubeba uzito, pamoja na bending strength - uwezo wa kujikunja). Lakini hivi vyote vinategemea chemical composition especially Carbon Content. Kwa kawaida nondo ili iweze kubalance hizo properties (bending &tensile) carbon content inatakiwa isizidi 0.3 %wt. Ikizidi inafanya chuma kuwa kiguma na kikikunjwa kinakatika (hakipindi).
Kinachotekea ni kwamba, hivi viwanda vyetu vinatengeneza nondo kwa kutumia vyuma chakavu kama spare za magari ambavyo vingi vinakuwa na carbon content kubwa (zaidi ya 4 %wt). Kwahiyo wakianza kuyeyusha carbon inakuwa juu sana, kwahiyo huwalazimu kuishusha mpaka ifike mpaka 0.3 %wt au chini zaidi. Lakini walio wengi inawachukua muda sana na pengine kushindwa kuishusha (zaidi ya 0.5 %wt) na kuamua kutengeneza tu nondo hivyo hivyo na matokeo yake ndo kukatika.Nondo hizi mara nyingi huchanganywa na ambazo zina ubora.
Kwahiyo, unataka kulishugulikia hilo tatizo, inabidi kwanza upime hivyo vitu hapo juu, TBS, then uende kwa huyo aliyekuuzia , yeye anafahamu hizo nondo alikozitoa (kiwanda).