Moseley
Senior Member
- Jul 10, 2010
- 187
- 98
Habari wana JF?
Kama kichwa cha habari kinavojieleza.
Kwa ufupi ni kwamba, naombeni msaada wa kisheria juu ya jinsi ya kupata hati ya eneo la zaidi ya hekari 18 ninalolimiliki kiasilia.
Nimekua katika harakati za kuyapatia hati maeneo ambayo ninayamiliki miaka nenda rudi. Maeneo hayo nimekua nikiyatumia kwa kilimo toka miaka ya zamani.
Kipindi cha nyuma babu yangu alikua anamiliki hilo eneo ambalo alimpatia baba angu sehemu ya eneo hilo ambalo kwa sasa ndo ninalolimiliki.
Mabwana ardhi wananambia sitaweza kupata hati ya maeneo hayo yenye zaidi ya hekari 18.
Naomba msaada wa kisheria, nifanyeje ili nipate hati ya miliki ya maeneo hayo?
Ni muda sasa nafatilia ila naambiwa sitaweza kupata kwa sababu eneo hilo lipo kwenye mpango mji. Sasa, eneo likiwa kwenye mpango mji maanake miliki asilia naikosa? Na kwa nn niikose haki yangu wakati maeneo hayo nayamiliki kihalali na hayana mgogoro wa aina yoyote ile?