Aputwike
Senior Member
- Aug 9, 2016
- 172
- 189
Nimeomba mkopo wa Tsh 1,500,000/= kutoka taasisi moja hapa nchini ambao riba yake ni 17%. Nimeweka dhamna kiwanja. Hivyo basi, nimeingiziwa huo mkopo ambao inatakiwa niulipe kwa muda wa miezi 6 ambapo kila mwezi inatakiwa nilope 300000. Lakini baada ya kuingiziwa pesa hiyo, nimeambiwa ni-deposit kwanza amana ya Tsh 202,500/= ambayo nitakuja kuichukua mwishoni baada ya kumaliza kurejesha huo mkopo. Kwa maana hiyo, kiasi nilichopata ni Tsh 1,300,000/=
Sasa jamani, naomba mnisaidie kukokotoa hapa. Je, huu mkopo una riba ya asilimia 17 kweli? Naomba msaada wenu
Sasa jamani, naomba mnisaidie kukokotoa hapa. Je, huu mkopo una riba ya asilimia 17 kweli? Naomba msaada wenu