Nimeona niongee machache leo kuhusu mzunguko wa pesa nchini

undugukazi

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2011
Posts
315
Reaction score
82
Nimeona niongee machache leo kuhusu mzunguko wa pesa nchini, kwa miezi ya karibuni kumekuwa na malalamiko na manunung'uniko mengi kwamba pesa imehadimika, naungana na wote wanaolalamika na nitajaribu kuja na solution moja kabambe lakini kwanza embu tujue wapi tumekosea? je majizi na mafisadi wamepungua? wala rushwa wamepungua? nways naamini wahusika wanaendela na utekelezaji wa kuhakikisha nchi ina nyooka. sasa tujikite kwenye solution.

Nimekaa nikawaza hivi mzunguko wa pesa ni nini? na je ni kodi kiasi gani inapotea kama mzunguko ni mdogo? nitajibu kwa mifano
kwa akili zangu za kawaida tu nikawaza kama dukani kwa mangi mtaani akiweza kuuza bidhaa zake na kulipa kodi inamaana wanaonunua watakuwa wamepata pesa mahali either kwa jasho lao au siyo ila ni pesa hizo na mangi atapeleka watoto shule akilipa ada, atanunua vifaa vya shule (kodi hiyo), wakiumwa atapeleka hopsital na atanunua dawa (kodi hizo), atamvalsiha mkewe mavazi safi na kumnunulia urembo na simu nzuri (kodi hizo), na huu mnyororo utaendelea hautaisha. sasa hii ni level ya duka na tukitumia rate za kodi zilizopo bila kuomba zipungue.

embu tafakari magari wananchi wanayoagiza nje ( mfano ukasema kodi iliyopo sana which is almost 50% ya CIF ikawa only 20% ya CIF nawaza kimakinikia hapa, then serikali ikafumba macho watu wakaagazia magari ya kifahari na yakibiashara inamaana serikali itapunjika sio? sasa turudi kwenye mapato ya serikali say yameingia magari 100000 ya cc 2000 yatakula mafuta kiasi gani kwa mwaka? watu wata ya pimp yatanunua bidhaa mbalimbali kama tairi au yakiharibika spare parties n.k (kodi hizo), na wale waliokuwa wanaogopa kuhonga magari watahonga mwisho wa siku serikali itakusanya zaidi ya ile asilimia 30 ya CIF iliyosamehe na mwitikio wa watu kununua magari utakuwa umeongezeka (kodi hizo).

twende kwenye starehe, sote tunafahamu msimu wa bajeti ni sekta gani inaongoza kwa kuletea mapato serikali? sitokusaidia kujibu kama haufahamu...sasa tafakari bia zinaanza uzwa jioni na kwanini sio mchana sa 6 angalau? (kodi hizo)


yapo mengi mnaeza ongezea ila cha kutafakari tu hata mafisadi wangepewa huruma tu ila kwa masharti waje wawekeze bongo na walindwe? nakumbuka nchi jirani hapo sitoitaja ila ni east africa waliwahi fanya kitu cha namna hiyo watu wenye pesa ziwe safi au chafu ukiwa ni mzawa serikali yao iliwaomba warudi kuwekeza home na waliwekeza vitu vya maana sana (kodi sana), badala ya kuwaonea wivu watu wenye pesa wapewe mazingira bora ya kwuekeza watoe ajira na kuleta mzunguko wa pesa nchini. nilwia kusikia tetesi sina uhakika eti leo hii ukiwa na pesa unaogopa hata kununua nyumba usije ukaulizwa umetoa wapi pesa

aisee mambo ni mengi ila tuongeze hapa chini njia za ksuababisha mzunguko wa pesa ( the great migration haihusiki lakini ingawa inaeza kuwa kweli inasaidia mzunguko wa pesa)

Asante
 
Kuachia mianya ya mafisadi ili pesa ionekane mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…