Nimeota leo Simba anafungwa na Azam kombe la Mapinduzi

handsome boy wa jf

Senior Member
Joined
Jan 2, 2022
Posts
163
Reaction score
350
Aiseee jamani wana simba leo naona kabisa tunafungwa leo na azam jana kuna ndoto nimeiota aisee nimeota naona vilio vimetawala msimbazi naona kocha pablo yupo airport amepanda ndege amefukuzwa naona leo chama yupo jukwanii amevaa jezi za yanga akiwapungia mkono mashabiki wa simba nimeota pia goli la azam litafungwa kwa makosa ya beki za za simba.

Nimeota pape sakho ataumia kipindi cha kwanza atatolewa nje nimeona leo game ya leo azam japo anashinda goli 2 kwa bila nimeoneshwa goli la pili la azam litafungwa kiutatauta sana.

Nimeonyeshwa mchezo wa leo utakuwa na vurugu kubwa mnoo tena mnoo
 
Nimeota yanga wamepanda boti la Azam na vifurushi vyao vya mabegi wakielekea Dsm baada ya kufurushwa na Azam
 
Endelea kuota ila ikifika mahali ukaona choo ndotoni usikitumie ni mtego.
 
Wewe ota tu ..
Game itakapoisha tutakuamsha
 
Mkuu hujachoka kuota tu? Umetoa boko kwenye mechi ya Simba vs Namungo
 
Hayo ndy madhara ya kulala bila Kula usiku.

Lazima uote ndoto za hovyo.
 
Endelea kuota dada utopolo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…