Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 972
Tazama nalikuwa usingizini naam usingizi wa maono. Tazama malaika muona vionwa akanijia na kunichukua mpaka uwanda wa juu wa nchi.
Akaniambia tazama, nami nikawaona wanaume wa nchi wenye nguvu wakiliziba tundu kwa kuweka mawe aina anuai. Baada ya kulijaza shimo kwa mawe wakaweka juu yake mfuniko mzito wa ratili kumi elfu. Mara baada ya hapo makufuli ya dhahabu yaliyozungushiwa majani ya kijani kibichi yakafungwa juu yake na makufuli hayo haukuna mwanadamu yeyote awaye atakayeweza kuyavunja.
Mara nikashtuka na kukuta mzee fulani mwenye hekima akanisogolea na kuniambia, mwanangu hiyo sio ndoto ni maono. Makufuli ni Rais Magufuli, tundu ni Tundu Lissu, majani ya kijani kibichi ni CCM, mfuniko ni kura za wananchi, mawe ya aina anuai ni mambo mema aliyotenda Rais Magufuli na kumfifisha na kumpausha Lissu na wapinzani wengine na wanaume wenye nguvu wanawakilisha wapiga kura wote.
Mwisho wa ndoto ukweli.
Amani Msumari
Tanga