Kuota Kufa hakumaanishi kufa moja kwa moja, japokuwa waweza kufa kibiashara, kielimu, kikazi, kiroho n.k ama ukafa kabisa. Lakini ndoto yako imekuonyesha kufufuka upya kama ishara ya mafanikio mapya baada ya jambo fulani kuharibika au kufa kabisa, kwahiyo ulitakiwa kusali baada ya kuamka ili kuijaribu hiyo roho kujua kama ilitoka kwa Bwana au kwa Ibilisi. Hatahivyo unatakiwa kuwa mvumilivu pindi mambo yatakapokuendea hovyo hovyo maana ukimtegemea Bwana yatafufuka upya na kustawi vizuri. Mimi niliwahi kuota kuwa mwanasheria mkuu wa serikali wa kipindi hicho amefariki, nikaonekana mwenye huzuni sana nikimhadithia mama yangu juu ya hicho kifo. Lakini nilipoamka niliikemea ile ndoto isitokee kwa mapenzi ya Bwana maana huyo mwanasheria aliahidi kutupatia ajira pindi tu ningehitimu masomo yangu ya chuo kikuu. Ajabu baada ya muda mfupi mimi kumaliza chuo, huyo Mwanasheria mkuu alijiuzuru kazi/wadhifa wake kwa misukosuko, bhasi nikaijua maana ya ile ndoto(kumbe kifo nilichoona kwenye ndoto kilikuwa ni kifo cha kazi yake au wadhifa wake).